Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kakolanya: Kukaa nyumbani sio poa

BENO Pict

Muktasari:

  • Namungo ilitangaza kuachana na Kakolanya, hivyo alirejea SBS ambako hawezi kucheza hadi msimu umalizike, alikiri endapo kama mchezaji hawezi kuzingatia miiko ya kazi inakuwa ngumu kulinda kiwango chake.

KIPA wa Singida Black Stars, Beno Kakolanya aliyekuwa anacheza kwa mkopo Namungo, amesema hakuwa na msimu mzuri kutokana na kucheza mechi saba na sasa yupo nje ya kazi, akisema kwake sio poa, japo hana namna kwani msimu umeshaisha.

Namungo ilitangaza kuachana na Kakolanya, hivyo alirejea SBS ambako hawezi kucheza hadi msimu umalizike, alikiri endapo kama mchezaji hawezi kuzingatia miiko ya kazi inakuwa ngumu kulinda kiwango chake.

"Kwa mchezaji kukaa bila kucheza inahitaji nidhamu ya juu, kuanzia mazoezi, muda wa kulala, kuzingatia chakula kwa kifupi kufuata programu zinazotakiwa ukiwa kambini," alisema Kakolanya na kuongeza;

"Binafsi kukaa muda mwingi nyumbani naona ni changamoto, kwani kuna maisha fulani ya kuchanganyika na wenzako, ushindani wa kujituma mazoezini tofauti na mazoezi binafsi yaani nakosa vitu vingi, ila pia imenifunza uvumilivu na kujua tofauti wa kuwa na kazi na ikitokea ukakosa kazi."

Mbali na hilo, aliwataja makipa wazawa na wageni ambao kwa msimu huu anawaona wamefanya kazi kubwa ni Moussa Camara wa Simba ana clean sheets 17, Djigui Diarra wa Yanga akiwa na 15, Patrick Munthari wa Mashujaa mwenye 13 na Yona Amosi wa Pamba Jiji anayemiliki 10.

"Kusema ukweli makipa wazawa kuna kitu kikubwa cha kujifunza vitu vya kiufundi kutoka kwa Diarra na Camara namna ya kucheza soka la kisasa, ndio maana kuna haja tuamke tunapopata muda kuchangamkia kozi zinazotolewa za ukocha," alisema Kakolanya na kuongeza;

"Mfano mzuri ni mshambuliaji wa JKT Tanzania, John Bocco alisoma kozi za ukocha kabla ya kujiunga na timu yake ya sasa alikuwa anaifundisha timu B ya Simba karudi tena kucheza, lazima ana kitu cha tofauti cha kusaidiana na wengine."

Alikumbuka wakiwa Simba na Bocco aliwahi kumshauri zikitokea kozi akasomee ili kuimarisha ubora wa kazi zake:"Boko aliniambia nisiwe napuuza kozi zinapotokea hasa nikiwa na muda wa kufanya hivyo, naamini tukifanya hivyo makipa wazawa kuna kitu tutakiongeza."