Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yaendelea kutakata kwa Mkapa

SIMBA wanajambo lao kimataifa, hivyo ndio unaweza kusema baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya RS Berkane mchezo wa kombe la Shirikisho Afrika uliochezwa uwanja wa Mkapa.

Bao walilopata kipindi cha kwanza likifungwa na Pape Sakho Simba ni kama liliamsha kiwango cha mastaa wa Simba hawakuridhishwa nalo waliingia kwa kasi kipindi cha pili na kuonyesha soka safi la pasi fupifupi.

Dakika ya 50 ya mchezo Kibu alimtengenezea pasi safi Bwalya ambaye alishindwa kutumia nafasi baada ya kupiga shuti jepesi lililokuwa mboga kwa kipa wa Berkane.

Simba waliendeleza burudani ya pasi fupi fupi na kuwaacha wapinzani wao wakisaka mpira kwa tochi.


MORRISON AIBUA SHANGWE

Pablo alifanya mabadiliko dakika ya 62 kwa kumtoa Kibu na nafasi yake ilichukuliwa na Bernard Morrison ambaye mpira wake wa kwanza kugusa ulikuwa hatari kwa RS Berkane.

Morrison alipiga shuti kali nje ya 18 ambalo liligonga mwamba na kurudi ndani na kuondolewa na mabeki wa timu pinzani.

Dakika ya 72 Mkude alipiga shuti kali nje ya 18 ambalo lilipanguliwa na kipa na kuzaa kona ambayo ilichongwa na Morrison lakini haikuwa na madhara kutokana na kuokewa.

Simba walifanya mabadiliko kwa kuwatoa Bwalya na nafasi yake ilichukuliwa na Mzamiru Yassin na walimtoa Sakho aliingia Peter Banda.

Wakati RS Berkane walifanya mabadiliko wa wachezaji watano alitoka Sofian Moudane nafasi yake ilichukuliwa na Mohammed Aziz, alitoka Ba akaingia Brahim El Bahraoui, pia walimtoa Tuisila Kisinda nafasi yake ilichukuliwa na Mohammed Farehane.

Pia alitoka Hamza El Mossaoui nafasi yake ilichukuliwa na Chadrack Muzungu Lukombe na walimtoa Mouad Fekkak nafasi yake ilichukuliwa Elmehdi Aubilla.

Mabadiliko hayo kidogo yalionyesha upinzani kwa Simba kwani RS Berkane waliweza kupata kona mbili lakini hazikuwa na madhara langoni mwa Simba.


BAO LA OFFSIDE LAZIA UTATA

Zimetumika dakika zaidi ya tano mpira kusimama kupisha virugu za benchi la RS Berkane waliokuwa wameingia uwanjani.

Dakika ya 84 Oubilla alifunga bao kwa kichwa lilikataliwa na mwamuzi wa pembeni akiashiria kuwa mchezaji huyo aliotea ndipo wachezaji na benchi la ufundi lilipomzonga mwamuzi huyo

Mpira baada ya kumalizika wachezaji na benchi la RS Berkane walionyesha kuto kulidhishwa na maamuzi ya waamuzi na kuanza kuwazonga askari walitumika kuwakinga.