Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yaanzia Dodoma, Kagere akiwapa furaha mashabiki

Muktasari:

Baada ya subiri subiri ya muda mrefu, hatimaye Simba wamefunga bao kwenye mchezo dhidi ya Dodoma Jiji na kuondoka na pointi tatu muhimu.

Baada ya subiri subiri ya muda mrefu, hatimaye Simba wamefunga bao kwenye mchezo dhidi ya Dodoma Jiji na kuondoka na pointi tatu muhimu.

Bao hilo limefungwa na mshambuliaji Meddie Kagere kwenye dakika ya 25 za kipindi cha pili sawa na dakika ya 70 ya mchezo, akiwanyanyua mashabiki wa timu hiyo.

Bao hilo amefunga kufuatia kuzembea kwa mabeki wa Dodoma Jiji kuokoa mpira wa juu uliokwenda langoni mwao.

Licha ya kufungwa kwa bao hilo, wachezaji wa Dodoma Jiji wamelalamikia bao hilo wakidai kabla ya kufungwa kulikuwa na kuotea kwa mchezaji wa Simba.

Shangwe la mashabiki wa Simba hatimaye likaanza uwanjani hapa ambapo muda wote wamesikika wakiliimba jina la Meddie Kagere aliyefunga bao hilo.

Kagere anafunga bao muhimu kwa Simba ambayo imekua na uhaba wa kufunga mabao tangu mchezo wao wa kirafiki dhidi ya TP Mazembe.