Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Mwinyi aahidi mamilioni Simba ikitwaa ubingwa CAFCC

Muktasari:

  • Hii ni mara ya pili kwa Klabu ya Simba kucheza fainali ya michuano ya CAF, baada ya kufanya hivyo kwa mara ya kwanza mwaka 1993 dhidi ya Klabu ya Stella Abidjan ya Ivory Coast. Katika mchezo huo, uliochezwa kwenye uwanja wa Uhuru (zamani Taifa) Dar es Salaam, Mgeni Rasmi alikuwa Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi na Simba ilipoteza katika mchezo huo.

Unguja. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameahidi kuizawadia Klabu ya Simba, Dola  za Marekani 100, 000 (Sh269 milioni) endapo itafanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Mechi ya Simba dhidi ya Berkane ya Morocco inatarajiwa kuchezwa kesho Jumapili saa 10: 00 jioni katika uwanja wa New Amaan Complex Zanzibar.

Katika mechi hiyo ambayo Rais Mwinyi atakuwa mgeni rasmi, pia amelipia gharama za uwanja ambazo ni asilimia 15 ambazo zilitakiwa kulipwa na Simba.

Dk Mwinyi ametoa ahadi ya kiasi hicho  alipokutana na kuzungumza na viongozi pamoja na wachezaji wa klabu ya Simba katika Hoteli ya Madinat Al Bahr jioni hii Mei 24, 2025.

Pamoja na ahadi hiyo, kiongozi huyo wa nchi amewatia moyo wachezaji na kuwatakia kila la heri kuelekea mchezo wao wa fainali.

"Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) zinaunga mkono juhudi za klabu ya Simba zilizowezesha kufikia hatua ya fainali," amesema

Amewahimiza wachezaji kucheza kwa kujiamini ili kutwaa kombe hilo kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo.

Pia Dk Mwinyi amewasihi mashabiki wa soka kuiunga mkono Simba kwa moyo mmoja na kuishangilia kikamilifu ili kuwapa hamasa wachezaji katika kutimiza ndoto ya kutwaa kombe la Shirikisho.