Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

JKU yaweka rehani taji la ZPL, KVZ yaizima KMKM

ZNZ Pict

Muktasari:

  • Kipigo hicho kwa JKU kilichopatikana jioni ya leo kwenye Uwanja wa Mao B, mjini Unguja kimeiweka timu hiyo katika hatari ya kulitema taji la ubingwa ililotwaa msimu uliopita.

MAAFANDE wa Mafunzo imekwea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Zanzibar (ZPL) baada ya kuizima JKU kwa mabao 2-1, huku KVZ ikiizima KMKM 2-0.

Kipigo hicho kwa JKU kilichopatikana jioni ya leo kwenye Uwanja wa Mao B, mjini Unguja kimeiweka timu hiyo katika hatari ya kulitema taji la ubingwa ililotwaa msimu uliopita.

JKU imesalia nafasi ya tano ikiwa na pointi 46 kupitia mechi 27, ikisaliwa na michezo mitatu ambayo ikishinda zote itafikisha pointi 55 tu.

Mafunzo ilipata mabao yake kupitia kwa Matheo Andrea dakika ya 45+3 na Rashid Abdallah dakika ya 57, huku la kufutia machozi la JKU likifungwa na Rashid Ali dakika ya 55.

Matokeo hayo yameifanya Mafunzo kupanda hadi kileleni ikiing'oa Mwembe Makumbi kwa kufikisha pointi 54 kupitia mechi 27. Mwembe Makumbi ina pointi 52 ikicheza mechi 26, ikiporomika hadi nafasi ya tatu kutokana na ushindi wa KVZ dhidi ya KMKM.

KVZ ilipata ushindi wa mabao 2-0 katika pambano jingine lililopigwa pia jioni ya leo kwenye Uwanja wa Mao A, Unguja na kufikisha pointi 53 kupitia mechi 27.

Mabao yaliyowazima Mabaharia wa KMKM yakiwekwa wavuni na Boniface Nickson dakika ya 44 na Michael Joseph aliongeza la pili dakika ya 66.

Ligi hiyo itaendelea tena keshokutwa Jumatatu, wakati mechi za raundi ya 27 zikipigwa kabla ya msimu kufikiwa tamati katikati ya mwezi ujao.