Simba yaanza kuwapima afya wachezaji wazawa

Muktasari:
- Huku wengine ambao hawakufanyiwa vipimo Aishi Manula, Mohammed Hussein 'Tshabalala', John Bocco, Kibu Denis na Jimmyson Mwanuke na wataungana kesho na mastaa wakigeni
Simba leo imewafanyia vipimo wachezaji wazawa katika hospital ya Taifa ya Muhimbili tayari kwa maandalizi ya msimu ujao wachezaji hao ni Ali Salim, Mzamiru Yassin, Israel Mwenda, Nassor Kapama , Habib Kyombo. Shomari Kapombe, Ahmed Teru Ferooz, Mohammed Mussa
Huku wengine ambao hawakufanyiwa vipimo Aishi Manula, Mohammed Hussein 'Tshabalala', John Bocco, Kibu Denis na Jimmyson Mwanuke na wataungana kesho na mastaa wakigeni
Mastaa wakigeni ambao watapimwa leo ni Clatous Chama, Jean Baleke, Sadio Kanoute, Peter Banda, Saido Ntibazonkiza, Joash Onyango, Moses Phiri, Pape Sakho na Henock Inonga na wachezaji wengine waliosajiliwa.