Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba na Azam hakuna mbabe

MCHEZO wa Ligi Kuu kati ya Simba na Azam umemalizika kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa kwa Sare ya bao 2-2.

Kipindi cha kwanza cha mchezo huo kilimalizika wa Simba kwenda mapumziko wakiongoza kwa bao 1-0 bao lililowekwa nyavuni dakika ya 27 na Mshambuliaji wa timu hiyo Meddie Kagere.

Katika kipindi hicho licha ya kumalizika wakiongoza lakini Simba watajilaumu kwa kushindwa kutumia vyema nafasi zaidi ya nne za kufunga zilizotengenezwa na wachezaji Clatous Chama, Rally Bwalya, Meddie Kagere, Luis Miquissone na Perfect Chikwende.

Kipindi cha pili kilirejea kwa timu zote mbili kucheza kwa utulivu huku Azam wakionekana kuamka taofauti na ilivyokuwa kipindi cha kwanza kwani walianza kupeleka mashambulizi kwenye lango la Simba.

Dakika ya 53 Simba kupitia kwa Chikwende walikosa bao la wazi baada ya kipa ishia mpira ambao angetulia angefunga ama kumpasia Miquissone ambaye pia alikuwa kwenye nafasi nzuri ya kufunga.

Azam wamefanya mabadiliko ya wachezaji wawili dakika ya 61 kwa kuwato Ally Niyonzima na Salum Abubakar na nafasi yake kuchukuliwa na Mudathir Yahya na Yahya Zaydi.

Dakika ya 66 Azam walisawazisha kupitia kwa Iddi Seleman aliyepiga shuti nje ya Boksi la 18 la Simba na kumshinda mlinda lango wa Azam Aishi Manula na mpira kuzama wavuni.

Dakika ya 68 Simba nao walifanya mabadiliko kwa kumtoa Perfect Chikwende na nafasi yake kuchukuliwa na Benard Morisson Pia dakika nne baadae Simba walimtoa Rally Bwalya na nafasi yake kuchukuliwa na Chriss Mugalu.

Dakika ya 76 Azam walipata bao la pili kupitia kwa Ayoub Lyanga aliyemalizia pasi safi ya Iddi Seleman na kufanya Azam kuongoza kwa bao 2-1 uongozi ambao haukudumu kwani dakika ya 78 Simba walisawazisha kupitia kwa Luis Miquissone aliyepiga shuti la mbali na kuzama nyavuni.

Dakika ya 86 kocha wa Simba Gomes Da Rosa alimtoa mfungaji wa bao la pili la timu hiyo Miquissone na nafasi yake kuchukuliwa na Mzamiru Yassin.

Dakika ya 90 alAzam walimtoa Prince Dube na nafasi yake kuchukuliwa na Never Tigere

Mpaka dakika 90 za mchezo huo zinakalizika Simba 2-2 Azam Fc.