Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mchakato wa mabadiliko Simba ndani ya siku 60

Muktasari:

Uchaguzi unaendelea kwa wagombea Juma Nkamia na Murtaza Mangungu na mawakala wao sanjari na kamati ya uchaguzi kuhesabu kura ambapo wakati wowote kuanzia sasa kamati ya uchaguzi huo itamtangaza mshindi.

Uongozi wa klabu ya Simba,  umesema suala la mabadiliko ya uendeshaji wa klabu linakwenda vizuri.

Taarifa ya klabu hiyo iliyotolewa leo kwenye mkutano mkuu imesema kwa mujibu wa sheria ya ushindani, wanatarajia suala la mchakato wa uwekezaji litakamilika ndani ya siku 60.

"Klabu ya Simba imepewa siku 28 ili kupeleka ufafanuzi juu ya muunganiko wa kampuni ambazo ziko kwenye mchakato huo na klabu inategemea kuwasilisha ufafanuzi huo Februari 10," imesema.

Kwa mujibu wa Taarifa ya klabu, muunganiko huo ni wa Simba Sports Club, kupitia kampuni tanzu ya Simba Holdings Limited na Mo Simba Holdings Limited.

"Baada ya kuomba idhini kwenye tume t a ushindani,  tume ilitoa tangazo Januari 9 kuhusu mchakato wa kuendelea kutoa nafasi kwa klabu ya Simba kupeleka utetezi  baada ya tume kutoa matokeo ya awali juu ya uchunguzi wao," imeeleza taarifa ya klabu hiyo iliyotolewa leo kwenye mkutano mkuu wa klabu uliokwenda sanjari na uchaguzi mdogo wa kuziba nafasi ya mwenyekiti wa klabu.

Imesema tume imetoa siku 21 kwa watoa pingamizi kuwasilisha maelezo yao juu muunganiko huo na klabu itapeleka ufafanuzi Jumatano ijayo.