Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba kufanya maamuzi magumu

Wachezaji wa timu ya Simba.

Muktasari:

Hata hivyo kocha wa Simba, Dylan Kerr huenda ndiye atakayekuwa na maamuzi magumu zaidi katika kukata wachezaji alionao, ambapo ametamka wazi kuwa hakuna nyota yeyote wa timu hiyo mwenye uhakika wa kusalia kikosini atakapopitisha panga wakati wowote kuanzia sasa.

CCM ilifanya maamuzi magumu kulitaka jina la Edward Lowassa. Naye Waziri Mkuu huyo mstaafu pia alifanya maamuzi magumu kuhama CCM na kutua Chadema na Chadema pamoja na Ukawa walifanya maamuzi magumu zaidi kumteua Lowassa kuwa mgombea wao wa nafasi ya Urais.

Hata hivyo kocha wa Simba, Dylan Kerr huenda ndiye atakayekuwa na maamuzi magumu zaidi katika kukata wachezaji alionao, ambapo ametamka wazi kuwa hakuna nyota yeyote wa timu hiyo mwenye uhakika wa kusalia kikosini atakapopitisha panga wakati wowote kuanzia sasa.

Muingereza huyo alisema nyota yeyote ambaye hajaonyesha uwezo wa kuvutia hata kama ni kutoka nje ya mipaka ya Tanzania atalazimika kukatwa na kupendekeza timu yake kufanya usajili mwingine ili kujiimarisha zaidi.

Kocha huyo aliendeleza kilio chake katika nafasi ya straika kwa kusema kuwa wale waliopo sasa wameonyesha uwezo duni na hawataweza kuiongoza timu hiyo kutwaa ubingwa msimu ujao.

Mastraika waliopo Simba kwa sasa ni Mganda, Hamis Kiiza na wazawa Ibrahim Ajibu, Mussa Hassan ‘Mgosi’, Danny Lyanga, chipukizi Boniface Maganga na Elius Maguli ambaye kuna madai kuwa huenda akatolewa kwa mkopo.

“Sina mfungaji, hilo liko wazi, wale waliopo sasa wanacheza kawaida sana, sidhani kama nahitaji kupiga kelele kila siku wakati hilo linaonekana wazi,” alisema Kerr.

“Nitafanya mabadiliko kiasi katika kikosi, nahitaji wachezaji 25 pekee hivyo kuna ambao itabidi tuwapunguze, hayo yote yanafanyika katika kipindi hiki cha maandalizi.

“Kuwa atapunguzwa nani na nani atabaki hilo siwezi kusema ila kikubwa ni kwamba hakuna aliye salama mpaka sasa, mchezaji yeyote anaweza kukatwa,” alisema Kerr.

Akiwazungumzia nyota wapya waliokuja kwa ajili ya majaribio klabuni hapo kipa Ricardo Andrade kutoka Brazil na straika Makan Dembele kutoka Mali, Kerr alisema atahitaji muda wa kuwatazama ili ajue kama wana nafasi katika kikosi chake ama la.

“Nawasubiri mazoezini, nataka waje niwaone ndipo nitafanya maamuzi kama wanafaa kusajiliwa ama la,” alisema Kerr.

Habari zaidi kutoka ndani ya Simba zinaeleza kuwa timu hiyo huenda ikawatoa nyota wake saba kwa mkopo kwenda klabu mbalimbali za Ligi Kuu ili kwenda kupandisha viwango vyao.

Nyota wanaotajwa kupelekwa kwa mkopo ni pamoja na straika Elius Maguli, kipa David Kisu na kiungo Michael Mgimwa ambao wote wanatolewa kutokana na ushindani mkubwa uliopo katika nafasi zao.

KIRAFIKI

Mara baada ya mechi yao ya Simba Day, Kerr ametoa mapumziko ya siku nne kwa wachezaji wake na Jumatano wataendelea na mazoezi huku wakitafuta mechi ya kirafiki Jumamosi ya wiki hii.

Rais wa Simba, Evans Aveva alisema wanatafuta mechi ya kirafiki kwa ajili ya kuendelea kujiweka fiti wikiendi hii lakini pia wanaangalia tena uwezekano wa kuiondoa timu hiyo Dar es Salaam kwaajili ya kambi.

“Tutacheza mechi ya kirafiki Jumamosi, tunatafuta timu kwa sasa ila baada ya hapo tutazungumza na kocha kuangalia tunaweza kufanya nini lakini sisi tunapendelea kuiondoa timu Dar es Salaam tena,” alisema.