Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yaibuka tena “hatujapewa fedha za ubingwa kwa misimu mitatu”

Muktasari:

  • Katika taarifa kwa umma iliyowekwa kwenye kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya Klabu ya Yanga, imeeleza hivi: “Tumeona taarifa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuwa inaidai Klabu ya Young Africans bila kutoa ufafanuzi wa deni lenyewe.

Baada ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutoka hadharani na kuijibu Yanga kuhusu madeni inayowadai, klabu hiyo imeibuka tena.

Katika taarifa kwa umma iliyowekwa kwenye kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya Klabu ya Yanga, imeeleza hivi: “Tumeona taarifa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuwa inaidai Klabu ya Young Africans bila kutoa ufafanuzi wa deni lenyewe.

“Tunapenda kuujulisha umma kuwa Klabu ya Young Africans haijawahi kulipwa fedha yoyote ya ubingwa wa Kombe la Shirikisho kwa misimu mitatu mfululizo (2021/2022, 2022/2023 na 2023/24).

“TFF wamekuwa wakishikilia fedha hizi za ubingwa kwenye akaunti zao kila msimu unapomalizika huku wakifahamu ni makosa na ni kinyume cha utaratibu.

“Hakuna uthibitisho wowote wa kimaandishi kuonyesha kama TFF wamewahi kulipa fedha hizi za ubingwa kwa Klabu ya Yanga.

“Ni aibu na fedheha na kumtia dosari mdhamini kuendesha mashindano bila kumlipa Bingwa kwa misimu mitatu mfululizo.

“Tunaelekeza, dawa ya deni ni kulipa kwa wakati ikiwa ni haki ya mshindi na inampa heshima mdhamini wa mashindano.

Yanga imesema kuhusu malipo ya ada za wachezaji wa kigeni ambazo TFF imesema kuwa klabu hiyo ilitaka zikatwe kwenye fedha hizo za ubingwa, malipo hayo ya ubingwa yalipaswa kufanyika msimu unapomalizika wakati malipo hayo ya wachezaji hufanyika mwanzo wa msimu.

Aidha Yanga imeendelea kusisitiza kulipwa pesa yake ya ubingwa wa Kombe la Shirikisho la CRDB kwa msimu wa 2023/24 ili waweze kukubali kucheza mchezo wa fainali ya msimu huu dhidi ya Singida Black Stars iliyopangwa kuchezwa Juni 28,2025 Uwanja wa Amaan, Zanzibar

“leleweke, ada za malipo ya wachezaji wa kigeni walizozisema kwenye taarifa yao hulipwa mwanzo wa msimu mpya na hela hizi za Ubingwa hutolewa Mwisho wa msimu.

“Klabu ya Young Africans haijawahi kupokea taarifa yoyote rasmi kutoka TFF kuhusu Klabu yetu kuwa na deni kwao.

“Uongozi wa Klabu ya Young Africans unaendelea kusisitiza kulipwa pesa yake ya Ubingwa wa Kombe la Shirikisho la CRDB, kwa msimu wa 2023/24 ili tuweze kucheza mchezo wa Fainali siku ya tarehe 28 Juni, 2025.”