Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba, Chipukizi ngoma droo

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba wametosha nguvu katika dakika 45 za kipindi cha kwanza dhidi ya Chipukizi ikiwa ni mwendelezo wa mechi za Kombe la Mapinduzi zinazochezwa Uwanja wa Amaan Kisiwani hapa.

Timu hizo zimekwenda mapumziko zikiwa sare ya bao 1-1 ambapo Chipukizi inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Zanzibar

Chipukizi walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 35 likifungwa na Faki Sharif ambaye aliwazidi ujanja mabeki wa Simba na kupiga shuti lilitinga nyavuni huku kipa wa Simba Beno Kakolanya akishindwa la kufanya.

Meddie Kagere aliisawazishia Simba bao dakika ya 44 akipokea mpira wa krosi uliopigwa na David Kameta 'Duchu' ambaye kipindi cha kwanza alicheza soka katika ubora wa juu.

Kabla ya bao hilo la kusawazisha Duchu alikosa bao dakika ya 41 baada ya mpira wa kupita pembeni mwa goli ikiwa ni sawa na dakika ya 45 ambapo pia shuti lake lilitoka nje.

Kipindi cha kwanza Simba ilikosa pia bao dakika ya sita baada ya Hassan Dilunga kupokea krosi ya Gadiel Michael ingawa shuti lake halikuwa na madhara kwa wapinzani wake.

Hata hivyo, dakika ya 25 Chipukizi walifanya shambulizi langoni mwa Simba lakini mabeki walikuwa makini kuokoa hatari hiyo.