Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Samatta, mastaa 18 Simba na Yanga kuipamba Alliance Day

ALLIANCE Pict

Muktasari:

  • Lengo la Alliance Day ni kuenzi maono ya mwasisi wa kituo cha michezo cha Alliance, James Bwire aliyefariki Januari 26, mwaka huu, pamoja na kusherehekea miaka 25 tangu kuanzishwa kwa shule za Alliance.

NAHODHA wa timu ya taifa, Taifa Stars, Mbwana Samatta pamoja na mastaa zaidi ya 18 wa Simba, Yanga na timu nyingine za Ligi Kuu Bara wanatarajia kushiriki na kunogesha tamasha la Kituo cha Michezo cha Alliance (Alliance Day) linalolenga kuenzi maisha ya mwasisi wa kituo hicho, James Bwire.

Tamasha hilo litafanyika Julai 9, mwaka huu kwenye Uwanja wa Nyamagana, jijini Mwanza ambapo Samatta na mastaa wengine kutoka Simba na Yanga wataunda timu ya pamoja (Kombaini) ambayo itacheza dhidi ya wachezaji waliowahi kupita kituo cha Alliance (Alliance All Stars). 

Mchezo huo utachezwa kuanzia saa 10 jioni, ukitanguliwa na matukio mbalimbali zikiwemo mbio za hisani zitakazohusisha wafanyakazi wa kituo hicho na wadau wengine, na mechi za watoto wa vituo vya kulea vipaji vilivyopo mkoani Mwanza.

Mwenyekiti wa Kituo cha Alliance kilichopo Mahina, jijini Mwanza, Stephano Nyaitati amesema hadi sasa wachezaji 18 wamethibitisha kushiriki tamasha hilo wakiwemo nyota wa Yanga, Prince Dube, Israel Mwenda, Djigui Diarra, Maxi Nzengeli, Salum Abubakar 'Sure Boy' na Jonas Mkude.

Wengine waliothibitisha kushiriki ni Novatus Dismas, ‎Mourice Abraham, ‎Hussein Kazi, ‎Said Ndemla, ‎Ladack Chasambi, ‎Yusuf Kagoma na Hassan Dilunga, wanaotarajiwa kuwasili jijini Mwanza Julai 8, mwaka huu.

Amesema mbali na kumuenzi James Bwire aliyefariki Januari 26, 2025, bonanza hilo ni maalum kwa ajili ya kusherehekea Jubilei ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa shule za Alliance ambazo zimezalisha mastaa mbalimbali wa soka akiwemo Israel Mwenda, Novatus Dismas, Yusuf Kagoma, Hance Masoud, Mourice Abraham, Aisha Masaka na Aisha Mnunka.

“Tunamuenzi na kusherehekea maisha ya mzee wetu Bwire (James) kwa sababu vijana wengi hasa wachezaji hawakaupata fursa ya kuja kumzika kutokana na kubanwa na ratiba za ligi, hivyo, waliomba wapate siku ya kuja kujumuika na familia na kusherehekea maisha yake,” amesema Nyaitati.

Amesema, malengo mengine ni kutumia nafasi hiyo kutengeneza mipango kwa ajili ya msimu ujao ikiwemo kuipandisha timu Championship na kukarabati miundombinu ya viwanja vyao ili kukidhi vigezo vya kuchezwa mechi za Ligi Kuu.

“‎‎Tuna vijana zaidi ya 200 ambao tunawasaidia tunawasomesha wanacheza mpira lakini hawalipi chochote, lazima tutafute mifumo itakayotuwezesha kituo kuendelea kuwa hai,” amesema Nyaitati.

Mmoja wa waratibu wa tamasha hilo, Jackson Mwafulango amewaomba wadau wa soka jijini Mwanza na mashabiki kukisaidia kituo hicho kufanikisha tukio hilo na kujitokeza kwa wingi kuwaunga mkono ili kuendelea kusaidia ndoto za vijana wengi wanaoitegemea Alliance.

‎‎”‎ ‎‎Tamasha tunalizindua mwaka huu na litakuwa endelevu kwa miaka yote, tumeamua tupambane lakini peke yetu hatuwezi tunaombea ushirikiano wa wadau mbalimbali katika kuhamasisha wananchi na wanamichezo kuja uwanjani kushiriki nasi,” amesema Mwafulango.