Simba bingwa Kombe la Mapinduzi 2022

Thursday January 13 2022
kombe pic
By Mwandishi Wetu

Simba imetwaa kombe la Mapinduzi 2022 baada ya kuifunga Azam FC bao 1-0 katika mechi ya fainali iliyopigwa Uwanja wa Amaan.

Bao la Simba limefungwa na Meddie Kagere kwa mkwaju wa penalti baada ya Pape Sakho kuchezewa madhambi ndani ya boksi na kipa Mathias Kigonya.

Simba inachukua kombe hilo kwa mara ya nne na ikivunja mwiko wa kutoifunga Azam kwenye fainali pindi wanapokutana baada ya kufungwa fainali tatu walizokutana.

Mechi hiyo iliyokuwa na ushindani mkubwa kwa pande zote kutafuta bao na kushinda kwa kujilinda.

Advertisement