Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sikia alichosema Kagoma Simba

KAGOMA Pict

Muktasari:

  • Kagoma katika mechi hiyo alilambwa kadi mbili za njano na hivyo chama lake kucheza bila huduma yake kwa muda mrefu kipindi cha pili cha mchezo, ambapo liliambulia sare ya kufungana bao 1-1.

UNAKUMBUKA kilichomkuta kiungo mkabaji wa Simba, Yusuf Kagoma katika ile mechi ya pili ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berkane iliyopigwa katika Uwanja wa New Amaan Complex mjini Zanzibar?

Kagoma katika mechi hiyo alilambwa kadi mbili za njano na hivyo chama lake kucheza bila huduma yake kwa muda mrefu kipindi cha pili cha mchezo, ambapo liliambulia sare ya kufungana bao 1-1.

Habari ikufikie kwamba kiungo huyo  mkabaji amesema kucheza fainali hiyo kumemjenga na kumpa akili mpya, huku akiahidi mabadiliko makubwa ya uchezaji kwa msimu ujao.

Kagoma amevaa medali ya CAF katika msimu wa kwanza kuitumikia Simba iliyomsajili kutoka Singida Fountain Gate baada ya timu hiyo kufika fainali hiyo na kupoteza mbele ya RS Berkane ya Morocco kichapo cha jumla cha mabao 3-1.

Akizungumza na Mwanaspoti, Kagoma alisema soka lake kiujumla limebadilika tangu alipojiunga na Simba kutokana na kukutana na aina tofauti ya maisha na timu alizowahi kuzitumikia kabla.

“Simba ni timu kubwa ina mashabiki wengi na ni timu shindani hasa katika masuala ya kuwania ubingwa soka la ndani, pia nimepata nafasi ya kucheza michuano ya kimataifa kwa mara ya kwanza kitu ninachojivunia, kwani imenipa akili mpya,” alisema Kagoma na kuongeza;

“Soka ni kujifunza kila siku mimi ni mwanafunzi bado naamini katika kupambana na kukubali kujifunda niwe muwazi nimeongeza vitu vingi kwenye uchezaji wangu naamini nitavifanya kwa vitendo msimu ujao.”

Kagoma alisema licha ya Simba kushindwa kufikia malengo ya kutwaa taji pamoja na mapambano makubwa waliyoyaonyesha kwake ni mafanikio makubwa kuvaa medali msimu wa kwanza.

“Haikuwa rahisi kutokana na kutokuwa na uzoefu kwenye michuano hiyo lakini nilikuwa na wachezaji viongozi kiwanjani walikuwa wananipa mbinu nini nifanye kwa wakati gani, najivunia kuwa sehemu ya kikosi kilichocheza fainali,” alisema na kuongeza:

“Najivunia mafanikio haya na naahidi msimu ujao nitakuwa bora zaidi na nitafanya kitu kikubwa kwa vitendo baada ya kujifunza kutokana na makosa niliyoyafanya naamini kuna mazuri pia nimeyaonyesha.”