Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Shule maalum ya vipaji vya michezo kujengwa Ilala

Dar es Salaam. Serikali inatarajia kujenga shule ya sekondari maalumu yenye vipaji vya michezo eneo la Mvuti wilaya ya Ilala ambayo itasaidia kuinua michezo mbalimbali nchini.

Mkuu wa wilaya ya Ilala, Mwilabuzu Ludigija akizungumza hayo wakati akizindua bwalo la gereza Kambi Mvuti, alisema itaanzishwa shule maalumu ya vipaji vya michezo na itajenga viwanja mbalimbali vya michezo ili watoto waweze kubitumia.
Ludigija alisema lengo la kujenga shule hiyo kuwafundisha watoto ili kupata vipaji maalumu  itakayosaidia kuinua michezo nchini ili washiriki kwenye makombe mbalimbali  ikiwemo mpira wa mguu.

"Hii shule itafundisha michezo mbalimbali itajengwa viwanja  mbalimbali vya kisasa ambavyo vitatumika kuwafundisha watoto watakaosoma katika shule hiyo na huo ni mpango wa serikali kuwa na shule maalumu za kufundisha vipaji vya michezo,"alisema Ludigija.

Afisa elimu Sekondari jiji la Ilala,Musa Ali alisema wana hekari 40 ambapo wanatarajia kuanzisha shule  ya sekondari kidato cha tano na sita pamoja na shule maalumu itakayochukuwa watoto wenye vipaji vya michezo.

Alisema fedha kiasi cha Sh 50 milioni imetengwa na halmashauri ya jiji hilo kwa ajili ya kujenga shule maalumu pamoja na viwanja vya michezo.

"Hapa tunasubilia fedha kiasi cha Sh50 milioni kutoka halmashauri tukizipata tu tutajenga viwanja vya mpira vya shule maalumu ya sekondari Mvuti ambapo hadi sasa hivi tumejenga mabweni matatu na madarasa 12," alisema Ally

Naye Mkuu wa gereza hilo Jastine Kipeta amesema wamezindua  bwalo la gereza Kambi Mvuti ambalo limegharimu kiasi cha Sh50 milioni  litatumika kwa shughuli mbalimbali ikiwemo burudani na sherehe.