Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serengeti Boys yachochea ile derby ya Arachuga

Muktasari:

  • Kocha wa Serengeti Boys, Oscar Milambo alisema michezo hiyo itawasaidia kukinoa kikosi chao vema na kuwaweka katika mazingira ya kimashindano mapema kabla ya kuelekea nchini Uturuki.

TIMU ya Arusha United “Wana Utalii” imejikuta katika wakati mgumu mara baada ya kushindwa kufurukuta katika safu za kikosi cha vijana wa Serengeti Boys katika mchezo wa kirafiki uliopigwa katika Dimba la Sheikh Amri Abeid na kutoka sare ya bao 1-1.

Arusha united iliona ni fursa kwao angalau kuomba mchezo wa kirafiki dhidi ya vijana hao kama sehemu ya maandalizi kuelekea mechi ya Derby ya Arusha dhidi ya AFC itakayopigwab mwishoni mwa wiki hii, lakini walijikuta wakishindwa kufanya kile walichotarajia ili kutuma salamu kwa wapinzani wao. nBaada ya kukabana kwa mda mrefu, Arusha United ndio ilitangulia kupata bao kupitia kwa Mshamu Saidy dakika ya 33 na kuwapeleka mapumziko wakiwa kifua mbele lakini kipindi cha pili, Kelvin John alirejesha heshima kwa Serengeti baada ya kusawazisha dakika ya 68.

Kocha wa Arusha United, Masoud Juma alisema wamefurahi kupata mchezo wa kirafiki dhidi ya Serengeti Boys kutokana ni timu kubwa inayowakilisha nchi kwenye mashindano ya kimataifa na wamevuna mengi kutoka kwa vijana hao ambayo endapo wakiyafanyia kazi uwanjani wataweza kutimiza malengo yao ya kupanda Ligi Kuu .

“Sijali matokeo kwa sasa bali kuwafundisha vijana wangu mbinu waliyokuwa wanatumia vijana hawa uwanjani kupata matokeo hasa mawasiliano yao lakini kikubwa vijana wetu wa Serengeti Boys wakazane kujituma zaidi kuhakikisha wanawapa furaha watanzania,” alisema Masoud.

Kocha wa Serengeti Boys, Oscar Milambo alisema michezo hiyo itawasaidia kukinoa kikosi chao vema na kuwaweka katika mazingira ya kimashindano mapema kabla ya kuelekea nchini Uturuki.

“Kuna baadhi ya vitu navigundua kupitia michezo ya kirafiki na natakiwa kufanya maboresho haraka kabla ya mashindano kuanza, hii yote ikiwa ni maandalizi.”