Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serengeti Boys moto wake hadi ubingwa U-17

Muktasari:

  • Serengeti Boys iko Kundi A pamoja na Angola, Nigeria na Uganda wakati Kundi B lina timu za Cameroon, Senegal, Morocco na Guinea

Dar es Salaam. Timu ya Taifa ya vijana ya Tanzania chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ inaanza kambi leo tayari kujiandaa na Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) kwa vijana yatakazoanza Aprili 18 mwaka huu hapa nchini.

Serengeti Boys iko Kundi A pamoja na Angola, Nigeria na Uganda wakati Kundi B lina timu za Cameroon, Senegal, Morocco na Guinea.

Pamoja na yote, Serengeti Boys imepania kufanya makubwa katika mashindano hayo huku wakiwataka wadau kuwapa sapoti ya hali na mali ili wajiandae vizuri.

Kwa kuonyesha kuwa hawatanii mapema Aprili mwaka jana walitwaa ubingwa wa mashindano ya Baraza la Soka kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) na Desemba ikatwaa ubingwa wa Cosafa.

Serengeti Boy ilitwaa ubingwa wa Cosafa kwa kuifunga Angola kwa penalti 6-5 baada ya sare ya bao 1-1 ndani ya dakika 90.

Msikie kocha sasa

Kocha wa Serengeti Boys, Oscar Mirambo anasema licha ya kufanya vizuri katika mashindano ya Cosafa mwaka jana lakini kuna baadhi ya changamoto inabidi zifanyiwe kazi ili timu ifanye vizuri katika mashindano ya Afcon mwaka huu.

“Pamoja na mambo mazuri ambayo vijana walifanya ikiwemo kutwaa Kombe la Cosafa la U-17, lakini kuna  bado changamoto ambazo tumeziona kwenye mashindano hivyo tunahitaji kuzifanyia marekebisho kwa muda huu tulionao ili tufanye vizuri.

“Tulikuwa katika kundi gumu ,kuna nchi kama Afrika Kusini hata kama haikupata nafasi ya kucheza nusu fainali lakini ni Taifa ambalo tayari limeshapiga hatua kubwa na mechi ambayo tulicheza nao ilikuwa kipimo  kizuri kwa vijana wetu kuona kwamba ni nini ambacho tunakifanya kwa usahihi na kitu gani ambacho mara zote tumekuwa tunakosea.

Anaongeza; “Angola tumepangwa nayo kundi moja kwenye Afcon hivyo tutakutana nao tena hapa. Ni timu bora lakini kwa kuwa tumeshakutana nao kwenye Cosafa hawatatupa shida kwenye Afcon. 

Kocha Mirambo alisema wako tayari kuikabili timu yoyote kwenye mashindano ya Afcon na hawana hofu na kila watakayekutana naye.

“Tunajiandaa kucheza na timu yoyote ambayo itakuwa kwenye kundi letu huku tukiwa tumelenga kuona tunakutana na zile timu ambazo tayari zimeshapiga hatua kubwa namaanisha kimaendeleo kuona kwamba ndio kipimo sahihi kwetu kwenda kushindana nao na kupata matokeo.

“Tunajipanga kwani tayari tumejua tuko na nani katika kundi moja na sasa tunapanga mikakati ya kuona ni kwa namna gani tunaweza tukafikia mafanikio ambayo ndio matarajio makubwa ya watanzania. 

“Changamoto kubwa ambayo tunatakiwa kuendelea kutatua kwenye timu ni lazima tuwe na usahihi kwenye kile ambacho tunataka kukifanya.

Pamoja na kujua uimara wa timu pinzani ambazo tunacheza nazo lakini bado tunahitaji kuwa na kitu ambacho kina ufanisi wa kutosha kwenye nguvu ambayo uko nayo.

“Sisi hatuna maumbo makubwa na hatuwezi kuwa na maumbo makubwa kwa muda ambao tumebakiwa nao.

Silaha kubwa ambayo tunayo ni kwamba muda wote lazima tucheze mpira wa kasi.Na ili ucheze mpira wa kasi uanhitaji kuwa na usahihi wa pasi unazopiga kwa sababu huwezi kuwa na spidi ya kukimbia muda wote”anasema Mirambo

Anaongeza: “Suala la mataifa mengine kuja na wachezaji wengi wenye maumbo makubwa ni kwamba kuwa na maumbo makubwa ni kitu kimoja lakini sio kitu pekee ambacho kitaipa uhakika timu kufanya  vizuri.

“Kama utainyima timu mpira wewe ndio unakuwa uko kwenye nafasi nzuri ya kupata matokeo pengine kuliko timu ambayo inakuwa haina mpira muda mwingi pamoja na kuwa na maumbo makubwa.

“Tumecheza na Angola, Afrika Kusini wana maumbo makubwa, tumecheza na Zambia ni warefu na wana maumbo makubwa lakini mwisho wa siku tulibakia kwenye kile ambacho tunakifanya vizuri na kuchukua ubingwa.

“Lazima ifike wakati tunatakiwa tuibadilishe  ile tafsiri kuwa mpira wa miguu sio tu mchezo bali tunapoingia uwanjani lazima tujue kuwa tunakwenda kushindana na tuufanye mchezo kama vita na tubakie kwenye vitu vya msingi ambavyo tunaweza kufanya vizuri na mwisho tuweze kupata matokeo bila kuangalia tunacheza na timu ya aina gani.” anasema Mirambo.

 Kambi

Tutaingia kambini Jumatatu (leo) lakini kulingana na program ambayo tulikuwa nayo, tuko nyuma ya muda hivyo tuna vitu vingi vya kufanya kwa muda mfupi.

“Tulikuwa na changamoto ya fedha ndio maana tumechelewa kuanza kambi.

“Hatuna wadhamini wa kutosha hivyo ni wakati wa kuhakikisha kama nchi tunaungana, tunashirikiana  na kutoa sapoti ili kuhakikisha vijana wetu wanaandaliwa katika  daraja la juu ambalo litatupa wote matumaini kwenye mstakabali wa maendeleo ya mpira wa miguu na kuitangaza nchi yetu kwa mataifa mengine,”anasema Mirambo.

Anaongeza: “Malengo yetu ni kucheza Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza kule Peru na ili kupata matokeo chanya lazima tujiandae. Niwaombe wadau wote ikiwemo serikali kuhakikisha wanatuunga mkono ili tuweze kufikia matarajio.

Mkurugenzi wa michezo hapa nchini, Yusuph Singo, anasema mashindano ya Uefa yatakayofanyia Uturuki yatawapa mazoezi mazuri wachezaji wa Serengeti Boys huku pia wakiendelea na mipango ya kuitafutia kambi nzuri ya mwezi mmoja timu hiyo kabla ya mashindano ya Afcon.