Serengeti Boys hesabu zote Uturuki

Muktasari:
Kocha Mkuu wa Serengeti, Oscar Milambo aliwahi kukaririwa akidai mechi hizo ni muhimu katika kutesti mitambo kabla ya kuliamsha dude kwenye Afcon U-17.
WENYEJI wa fainali za Afrika kwa Timu za Vijana U-17, Afcon itakayofanyika nchini Aprili mwaka huu, wanasubiri kuelekea kuonyesha makeke ya kunoa makali Ulaya kujiweka fiti zaidi kwa michuano hiyo.
Serengeti Boys, ilipokea mwaliko wa kushiriki katika mashindano ya kimataifa Uefa Assist ili kuzidi kujiweka fit inayaochezwa Machi, huku ikipangwa na Guinea, Uturuki na Australia.
Kundi la pili lina timu za Morocco, Cameroon, Uganda na Belarus wakati jingine lina timu za Senegal, Nigeria, Angola na Montenegro.
Kocha Mkuu wa Serengeti, Oscar Milambo aliwahi kukaririwa akidai mechi hizo ni muhimu katika kutesti mitambo kabla ya kuliamsha dude kwenye Afcon U-17.
“Tunakutana na timu ngumu ambazo zipo vizuri katika uwekezaji kwenye soka la vijana. Wachezaji wangu watapata motisha na uzoefu zaidi kuelekea katika maandalizi ya Afcon,” alisema.