Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sarri kasema bado yupo sana Chelsea

Muktasari:

  • Unajua alichojibu? Akaaambia hivi, bado yupo sana hawezi kung’oka Stamford Bridge licha ya mashabiki kupiga kelele za kumtaka awaachie timu yao.

LONDON, ENGLAND.KUNA watu wana masihara sana. Si wakamuuliza kocha wa Chelsea, Maurizio Sarri kwamba kwanini asiaachie ngazi tu baada ya timu yake kupata ushindi wa tabu sana mbele ya wachovu Cardiff City.

Unajua alichojibu? Akaaambia hivi, bado yupo sana hawezi kung’oka Stamford Bridge licha ya mashabiki kupiga kelele za kumtaka awaachie timu yao.

“Hapana, tena hapana. Nataka kubaki mahali hapa.

“Wakati nilipokuja hapa, timu ilikuwa imeachwa pointi 30 na Man City, ipo kwenye nafasi ya tano huko. Nataka kubaki hapa na kurekebisha mambo . Kuna tofauti kubwa kati ya Man City, Liverpool na sisi. Tunajaribu kupambana na kufanya kazi.