Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sampdoria, Atalanta macho kodo kwa Olunga

Nairobi. Mshambuliaji wa kimataifa wa Kenya ‘Harambee Stars’ na klabu ya Girona ya Hispania, Michael Olunga yupo mbioni kujiunga na miamba ya Italia Sampdoria na Atalanta.

Kwa mujibu wa taarifa za tetesi za usajili kutoka nchini Italia, zinasema klabu ya Sampdoria na Atalanta zinapigana vikumbo kutaka saini ya mchezaji huyo ambaye katika msimu uliomalizika wa La Liga, aliitumikia Girona FC, kwa mkopo akitokea Guizhou Hengfeng Zicheng ya China.

Kwa mujibu wa habari hizo za kuaminika, Mwanaspoti imedokezwa kwamba, Sampdoria tayari wameshaanza harakati za kuinyatia saini ya Olunga huku wakiwa na lengo la kuwapiku Atalanta ambao nao wanamvizia Straika huyo mwenye urefu wa sentimita 190.

"Olunga ni mmoja wa wanasoka wanaoviziwa na klabu ya Sampdoria na Atalanta. Straika huyu mwenye kasi, nguvu na uwezo mkubwa wa kutikisa nyavu alikuwa pale Girona kwa mkopo akitokea Guizhou Hengfeng," liliripoti gazeti la Calcio Mercato. 

Licha ya kucheza mara nyingi akitokea benchi, akiingia uwanjani dakika 426 tu, Olunga alifanikiwa kuifungia Girona mabao matatu na kutegeneza bao moja na kuthibitisha uwezo wake. Ikumbukwe kuwa nyota huyo aliifungia klabu yake hiyo hat-trick pekee ya msimu wa 2017/18.

Nyota ya Olunga ilianza kung'ara akiwa Gor Mahia kabla ya kutimkia nchini Sweden ambako alifunga mabao 12 na asisti nne na kuwavutia Wachina ambao walimwaga kiasi cha Ksh 467 milioni kuipata saini yake, lakini baada ya miezi ya kukaa nchini China alipelekwa Girona kwa mkopo.