Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sakho, Mhilu wapewa Dodoma

Muktasari:

Baada ya kuingia kutokea benchi na kubadilisha hali ya mchezo uliopita ugenini dhidi ya Biashara United, wachezaji Ousmane Sakho na Yusuph Mhilu wameanzishwa dhidi ya Dodoma Jiji.

Dodoma. Baada ya kuingia kutokea benchi na kubadilisha hali ya mchezo uliopita ugenini dhidi ya Biashara United, wachezaji Ousmane Sakho na Yusuph Mhilu wameanzishwa dhidi ya Dodoma Jiji.

Sakho ambaye alisababisha penati kwenye mchezo dhidi ya Biashara dakika za nyongeza, amepewa nafasi ya kuanza leo kwa lengo la timu kufunga bao mapema kwenye mchezo huu.

Kwa upande wake Mhilu, huu ni mchezo wake wa kwanza anaanzishwa, tangu aliposajiliwa na Simba hususani kwenye michezo rasmi ya timu hiyo msimu huu.

Pamoja na hao, Kocha Didier Gomes wa Simba, ameanza na kipa Aishi Manula, huku Israel Patrick akicheza beki ya kulia kutokana na Shomary Kapombe kuwa majeruhi. Mchezo uliopita, Israel alianzishwa beki ya kushoto.

Upande wa kushoto ni Mohammed Hussein, mabeki wa kati ni Pascal Wawa na Kennedy Juma, kiungo wa ulinzi ni Tadeo Lwanga.

Mhilu anacheza kama winga wa kulia wakati winga wa kushoto ni Hassan Dilunga. Kiungo wa kati Mzamiru Yassin huku Chris Mugalu akirejea kikosini na atasaidiwa na Ousmane Sakho.