Sakho aumia, Bwalya ambadili

Muktasari:
Dakika 10 tu zimetosha kwa nyota mpya wa Simba, Ousmane Sakho kucheza uwanjani, baada ya kuumia.
Dakika 10 tu zimetosha kwa nyota mpya wa Simba, Ousmane Sakho kucheza uwanjani, baada ya kuumia.
Majeraha ya Sakho yametokana na purukushani kati yake na David Ulomi wakati wakiwania mpira uliotokea upande wa kulia kwa Simba.
Kuumia kwa Sakho ni pigo kwa Simba ambao walitarajia nyota huyo awapatie kasi zaidi ya mchezo kutokana na uwezo wake mkubwa wa kutumia kasi.
Nafasi yake imechukuliwa na kiungo Rally Bwalya ambaye anakwenda kucheza nyuma ya Chris Mugalu.
Kabla ya kuingia kwa Bwalya, alionekana Meddie Kagere kama ambaye alitarajiwa naye aingie akiwa amenyanyuliwa lakini akaingia Bwalya.
Mchezo kati ya timu zote mbili (Dodoma na Simba) umeanza kwa kasi kubwa ambayo inamaanisha kila timu inataka kupata bao la mapema.
Manula aongeza utata nahodha msaidizi Simba
Kitendo cha kipa wa Simba, Aishi Manula kuvaa kitambaa cha unahodha kwwnye mchezo dhidi ya Dodoma Jiji, umeendeleza utata wa unahodha msaidizi.
Kwa misimu miwili iliyopita, Nahodha msaidizi wa Simba alikua ni Mohammed Hussein ambaye hata hivyo ameonekana kwenye mechi kadhaa msimu huu kutoendelea tena kuvaa kitambaa hicho.
Hussein ambaye ni beki wa kushoto wa Simba, amekuwa havai kitambaa cha unahodha kama nahodha mkuu John Bocco anapokosekana uwanjani.
Lakini hivi sasa pindi Bocco anapokuwa hachezi kitambaa hicho kimekua kikivaliwa na Shomary Kapombe kwenye mechi za msimu huu.
Kutokana na kutokuwepo kwa wachezaji wote wawili (Bocco, Kapombe), na wakati ambao Hussein yupo uwanjani, kitambaa hicho kimevaliwa na Aishi Manula.
Jambo hilo ndo limeongeza utata wa beki Mohammed Hussein amevuliwa kabisa majukumu ya kuwa nahodha msaidizi japo Simba hawajawahi kulitolea ufafanuzi