SABABU YA BARBARA GONZALEZ KUTEULIWA CEO SIMBA NI YANGA

Muktasari:
Uteuzi wa Barbara Gonzalez kuwa CEO Simba umeshika mitandao. Luqman Maloto anasema yule ndio kiboko wa Yanga. Dk Levy hajawahi kukaa kimya.
UTEUZI wa Barbara Gonzalez kuwa CEO Simba umeshika mitandao. Luqman Maloto anasema yule ndio kiboko wa Yanga. Dk Levy hajawahi kukaa kimya.
LUQMAN: Daktari, kati ya Yanga na Ihefu ipi timu kali? Yanga walipigwa 4-1 na Simba, lakini Ihefu wamefungwa na Simba 2-1 kwa taabu sana.
DK LEVY: Kali Ihefu. Acha kuifananisha Ihefu na wahuni wa Jangwani. Kumbuka goli zao mbili zimekataliwa na mshika Kibendera wa Msimbazi. Mashabiki wa vibandaumiza walikereka mpaka walipokuja kuburudika na unyunyu wa Tuisila.
Sikushangaa kabisa Mbumbumbu FC kulilia kumtazama Tuisila. Mahaba ya ufundi wa soka yalipitiliza uwezo wao wa kufikiri, kuamua na hisia. Kama mtu wa soka lazima useme ‘Shikamoo Tuisila’. Kwa uwezo wake na siyo kwa uzee wake kama Mzee Onyango. Onyango anawapa tabu tu kina Mkude kumuamkia kila siku kambini kama Mwalimu wa nidhamu Madenge Primary School. Tuisila ni shikamoo ya kipaji na uwezo.
Ndivyo ilivyokuwa kwa Ronaldinho Gaucho pale Saintiago Bernabue miaka ilee ukiwa bado unasoma Bwiru Sekondari huko Mwanza. Baada ya kuwalaza na viatu mastaa wenye ustaa halisi wa Real Madrid wakiongozwa na Zinedine Zidane Zizzou ‘Mchawi wa Kiarabu toka mitaa ya Paris’. Wakati ‘Mejishiani’ Dinho akitoka uwanjani majukwaa yote ya ‘Santiago Benabuu’ yalisikika makofi kutoka kwa wanazi wa ‘Madritisa’ wakisaluti kwa uwezo wake.
Heshima hii ya mashabiki kusimama majukwaani na kumpigia makofi mchezaji wa timu pinzani. Kwa hapa Bongo huu utamaduni umetuacha mbali sana. Haiwezi kamwe kutokea. Ila moyoni wataishia kukubaliana na hali halisi na kuishia kupata vidonda vya tumbo. Kuna wakati unamtazama Tuisila, unaona kama anawaonea wenzake au amelazimishwa kucheza nao. Alikuwa tofauti Sana Sana Sana Sana. Alikuwa juu kileleni pale Mawenzi kama siyo Kibo. Wenzake wakifagia vipisi vya sigara kwenye viunga vya Moshi mjini. Akiwatazama kwa chini. Ni kama aliwaweka wenzake chini ya soksi. Mchezo mzima ulichezwa kumzunguka yeye tu. Anatuliza mpira tofauti na wenzake. Anapiga pasi tofauti na wenzake. Na hata namna anavyogeuka kutazama wapi apeleke mpira ni tofauti sana. Aligeuka tofauti na wenzake. Ufundi huu ulikuwepo nyakati za kina Hussein Aman Masha, James Tungaraza ‘Bolizozo’, Clement Kahabuka, Mao Mkami ‘Mtaalamu’ baba yake siyo huyu moto mnayemuita Himid Mao. Na kina Steven Mussa. Hawa ndo walifanya anayofanya Tuisila wa leo. ‘TK Master’ kafanya watu wamuone Lunyamila wa 1993 na Steven Mapunda wa 1999 na Dua Said wa 1994. Tuisila alikumbusha Athuman China wa 1991 na Ramadhan Lenny wa 1993. Kuna zama huwa zinajirudia kupitia kiumbe. Tuisila katurudishia burudani ya miaka 27 nyuma. Kwa taarifa yako mashabiki wa jukwaa la mzunguko kipindi cha pili. Kwa mapenzi yao wenyewe bila kulazimishwa na mtu. Kwa utashi na mahaba yao huku nyoyo zao zikiwa zimefurahishwa mno. Walitoka nje ya uwanja kabisa na kuanza kukata tiketi kuingia kwa mara ya pili upyaaaaa. Kile kiingilio waliona kabisa wanamdhalumu Tuisila. Yule siyo mchezaji wa kumtazama kwa elfu tano. Tunataka mchezaji wa kimataifa aina ya Tuisila kama tunataka soka letu likue. Lakini hawa wanaopambwa kama mabibi harusi kwenye vyombo vya habari. Ni wachezaji sawa, lakini kwa Tuisila ni kama mtende kuota Jangwani. Anaonekana peke yake uwanja mzima. Mungu mbariki ‘TK Master’ fundi wa Kikongo aliyekuja kama mzimu Bongo. Asante Mungu kwa kutuletea kiumbe huyu.
Tuisila kama Tuisila. Niambie Morrison alikuwepo Mbeya?
LUQMAN: Huyo Tuisila wako alifanya nini mbele ya Tanzania Prisons? Usifanye ‘maskhara’ na wajelajela wa Mbeya waliojikita Sumbawanga. Mapokezi yote yale, kubebana kote kule, Yanga wakatulizwa na Prisons.
DK LEVY: Nasimama na Kigwangalla kwenye vitu siriazi. Naona unaongea mataputapu wakati akaunti yenu inasoma sufuri bin sifuri. Ninyi siyo matajiri. Naona jamaa kaleta totozi ije ‘kudraivu shops’ nzima. Chibu Dangote hajaiona? Mkimualika tena Mondi kwenye vishughuli vyenu kuna jambo linaweza kutokea. Ile ndo mikato ya mhuni wa Tandale yule. Na juzi nimemuona kocha wenu namna alivyovimba vimba usoni.
LUQMAN: Unamzungumzia MO ambaye ameifanya Simba kuwa tulivu, imechukua ubingwa mara tatu mfululizo, imeifunga Yanga 4-1. Au unamzungumzia MO yupi? Yuleyule MO aliyetamkwa na Forbes kuwa bilionea kijana zaidi Afrika? Ni MO ambaye pesa zake zimemng’oa Morrison Yanga akatua Simba? MO aliyeiwezesha Simba kucheza robo fainali Klabu Bingwa Afrika?
DK LEVY: Kwa wajuzi wa soka mechi ya juzi wanashindwa kuelewa. Ni mchezaji gani wa gharama pale Simba? Morrison au Mzamiru? Kama kuna mtu alitaka kusajili mchezaji angeangalia ile mechi hakuna ambaye angemtazama Morrison. Na siku zote inakuaga namna hii. ‘Bai ze wei’ siku hizi haitwi Mo tena. Kina Mo wanabaki kina Mo Sallah na Mo Ibrahim. Huyu wa kwenu aitwe tu Mwamedi au Mudi. Maana anachambana ‘twitani’ balaa. Matajiri huwezi kuwakuta wanafanya hizo mbishe. Tajiri unalilia kupoteza simu badala ya ‘kukrosi cheki’ na watengenezaji wa hizo simu ili wakurudishie kila kitu? Utajiri wa kikanjanja tu.
LUQMAN: Sasa hapo wewe unaumizwa na nini? Morrison kucheza Simba au MO kumwaga mpunga uliomleta Morrison Simba. Anakuumiza nani sasa? MO au Morrison? Unajua kama Morrison naye ni MO sema yeye kaamua kubaki na cheo cha wakili msomi aliyeishinda Yanga kwenye kesi ya usajili. Sema ukweli wa moyo wako, umeumia MO kusema Kigwangalla alimuomba mkopo wa bodaboda au kero yako ni MO kuwa tajiri sana?
DK LEVY: Sasa naumiaje? Akiuliziwa 20 bilioni tu anarusha mateke. Halafu unataka kujifanya wewe Simba saaana kuliko Kigwangalla? Unaongelea mikopo ya vibodaboda, tukutajie mikopo ya Mudi kwenye vibenki mjini hapa? Narudia tena yule CEO wenu yule. Endeleeni tu kumualika Dangote.
LUQMAN: Naona mnatumia nguvu nyingi sana kuuponda uteuzi wa Barbara Gonzalez, hamuangalii mauwezo yake, mnataka kumpima kwa jinsia yake. Kuza fikra, waza chanya, Barbara ndio CEO wa Simba na atafanya makubwa mengi hamtaamini.
DK LEVY: Yes hata Wema alikuwa mkurugenzi wa Handless, Asha Baraka ni bosi wa Twanga Pepeta. Wapo kina Madam Rita na wenzao. Huyu alikuwa PA wa Mudi tu hana historia nzito. Acha siasa muulizeni Mudi bilioni 20 ziko wapi?
LUQMAN: Barbara amefanya mengi, mafanikio ya Simba leo, Barbara yupo nyuma yake.