Rwanda huenda wakaikosa Canaf 2021

Mabingwa wa mashindano ya soka la walemavu Afrika Mashariki ya mwaka 2019, timu ya taifa ya Rwanda huenda hakaikosa michuano ya Canaf mwaka huu yanayofanyika nchini Tanzania.

Akizungumza na Mwanaspoti Katibu wa Shirikisho la soka la Tanzania kwa watu wenye ulemavu TAFF Moses Mabula amethibitisho hilo na anasema kuwa maandalizi ya michuano hiyo tayari yamekamilika kwa asilimia kubwa.

"Timu kumi na tatu tayari zimeshawasili hapa nchini isipokua timu ya taifa ya Nigeria ambao muda wowote kuanzia sasa wanatarajiwa kuingia hapa nchini"

"Lakini timu ya taifa ya Rwanda bado hawajawasili na kunauwezekano mkubwa wa kutoshiriki michuano hii kutoka na sababu zilizonje ya uwezo wao kwani mpaka sasa bado hawajawasili nchini" amesema Mabulla

Aidha pia Katibu huyo amethibitisha kuwa kuiona Tembo Warriors ni bure hivyo amewaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa Uhuru kuipa sapoti timu yao ya Taifa.

"Maandalizi ya timu yetu ya taifa yako vizuri kocha na bechi lake la ufundi pamoja na wachezaji wapo katika hali nzuri kikubwa nachowaomba watanzania ni kujitokeza kuipa hamasa timu ya ya taifa kwani ni bure hakuna kiingilio". Amesema Mabulla

Tembo Warriors wanatarajia kufungua pazia la michuano hii leo saa 9:00 alhasiri katika uwanja wa Uhuru watakapocheza na Timu ya Taifa ya Morocco.