Rais Samia aagiza viongozi Yanga kumaliza sakata la Fei Toto

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi wa Yanga kumalizana na mchezaji Feisal Salum ambaye ana mgogoro na timu hiyo.

Fei Toto ambaye amekuwa nje ya uwanja tangu Desemba mwaka jana kwa nyakati tofauti amekuwa kwenye viunga vya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) akishinikiza kuondoka timu hiyo huku uongozi ukimtaka kufuata utaratibu.

Rais Samia akipokea ombi la Yanga kuongeza eneo la kwa ajili kujenga uwanja wa kisasa Kaunda ametoa ombi kwa Yanga kumaliza sakata hilo.

“Viongozi wa Yanga nina ombi kwenu, sifurahii kusikia mnakuwa na mizozo na wachezaji, na sitaki kusema mengi, nataka niwaambie tu, hii ishu ya Fei Toto, hebu kaimalizeni.

"Kaimalizeni ili tuangalie mbele sasa, haipendezi klabu kubwa kama hii iliyofanya kazi nzuri, mnakuwa na ka ugomvi na katoto,"

"Hebu kamalizeni mwende vizuri. Nitasubiri kupata mrejesho wa hili, siku yoyote mkiwa tayari karibuni nyumbani mje kunipa mrejesho,”  Rais Samia