Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais FUFA aeleza Ligi Kuu Bara inavyotoboa Afrika

RAIS wa Shirikisho la Soka la Uganda (FUFA), Moses Magogo amefichua kwanini Ligi Kuu Tanzania Bara imepiga hatua kubwa na kuwa ya kishindani kwa miaka ya karibuni wakati ligi za Kenya na Uganda zikidorora.

Shirikisho la Kimataifa la Historia ya Soka na Takwimu (IFFHS) mwaka huu liliitaja Ligi Kuu Tanzania Bara kuwa kwenye tano bora ya ligi yenye nguvu Afrika na ya 38 duniani, kitu ambacho kimemsukuma bosi huyo wa Fufa kuzungumza akilinganisha na kasi hafifu ya ligi za Kenya na Uganda.

Kwa mujibu wa Pulse Sports, Magogo amesema Tanzania imejitangaza zaidi kupitia klabu za Simba na Yanga.

“Tanzania ni kama ipo dunia nyingine, inafanya vitu ambavyo sisi hatufanyi," alisema Magogo.

"Ni hicho tu. Kenya kuna timu kama Gor Mahia na  AFC Leopards ni wapinzani. Ili Ligi iwe bora, klabu zetu zinapaswa kuwa na upinzani. Tulikuwa na Mashemeji derby, ilikuwa nzuri sana. Uganda kulikuwa na Villa na Express zilizokuwa na nguvu. Uganda tulikuwa na Simba - Yanga na sisi kipindi hicho na mashabiki walikuwa na upinzani mkubwa."

Magogo anaamini kingine kinachoifanya Ligi Kuu Tanzania kupiga hatua kubwa kwa kulinganisha na nchi za Kenya na Uganda kwa miaka ya karibuni ni kuwapo kwa haki za televisheni, ambapo zimefanya mechi za ligi hiyo kuonyeshwa na kujiongezea umaarufu.