Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Popadic: Tumelalalia ndizi mbivu tatu na maji, naondoka Singida United

Muktasari:

 

  • Singida United kwa sasa ipo nafasi ya tatu kutoka chini ikiwa na pointi 32, baada ya kucheza michezo 27.

Singida. Kocha wa Singida United, Msebria Goran Popadic amesema siku timu yake ilipocheza na Prisons hatukunywa chai wa kula chakula cha mchana, usiku tulibahatika kupata ndizi tatu mbivu, tukala…tukanywa maji, tukalala.

Kutokana na hali hiyo ngumu kocha Popadic ameupa siku tisa uongozi wa Singida United kumlipa stahiki zake zote vinginevyo atavunja mkataba na kurejea nyumbani kwao.

Akizungumza na Mwanaspoti online leo nyumba kwake alisema asipolipwa hadi Machi 15 mwaka huu, ataacha kazi ya kurudi kwao Serbia.

Alisema licha ya kutokulipwa mshahara na marupurupu ya mwezi uliopita bado hajatimiziwa matakwa ya mkataba wake kuwa wangepewa gari, mpishi na mhudumu wa usafi, vyote hivyo hadi sasa wavijatekelezwa.

Kocha Popadic, alisema kwa sasa yeye na mwenzake wanishi maisha magumu kupindukia na mazingira ya kazi yamekuwa magumu.

“Kwa vile hatuna fedha kabisa hata ya kulipia bajaj kwenda uwanjani katika mazoezi ni shida, upatikanaji wa chakula ni tatizo kubwa tulilonalo kwa sasa.”

Msebria huyo alisema wanawashukuru majirani zao kwa kitendo chao cha kuwapa misaada ya chakula mara kwa mara. Kwa ujumla kwa sasa hawana uhakika wa kupata milo mitatu inayohitajika.

Aidha, Popadic alisema kwa wachezaji hali ni mbaya pia, walipwistahiki zao kwa miezi kadhaa na upatikanaji wa chakula kwao ndio shida zaidi.

“Wakati naanza kuifundisha timu hii Januari mwaka huu, nilikuta wachezaji saba wa kutoka nje ya nchi. Wote uwezo wao hauzidi wa wachezaji wa humu Tanzania. Kutokana na uhaba wa fedha, wengi wa wachezaji hao kutoka nje ya nchi, wametoroka timu. Pia hali kadhalika, wachezaji wa humu nchini wamekuwa wakiimbia timu mara kwa mara….shida ni njaa kali.”

Kocha huyo alisema rais wa timu Mwigulu Nchemba na meneja wake Festo Sanga wanaishi jijini Dar es Salaam. Kwa hiyo hawawezi kufahanu vizuri matatizo ya timu yao.

“Kwa kifupi hapa Singida United hakuna mshahara wala uwanja wa kufundishia timu (no salary no ground). Mimi sio mtu wa maisha ya ‘zig zag’…mimi nipo imara. Nisipopata haki zangu zote, narudi nyumbani bila shida. Toka nimeanza kazi hii ya ukocha nchi mbalimbali za Ulaya na Afrika, zijakumbana na maisha mabaya magumu kama haya niliyonayo kwa sasa,”alisema Popadic.

Meneja Singida United, Sanga amekiri kuwa timu inadaiwa na kocha na wachezaji, lakini sio kwa miezi nane kama inavyozungumzwa. Kadri uwezo unaporuhusu, tutaendelea kutatua changamoto hizo.

Shabiki mkubwa wa Singida United, Hango Steven alisema hekima na busara hazijatumika katika kuajiri makocha toka Ulaya, wakati timu haina mbele wala nyuma katika masuala ya uchumi.