Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Polisi Tanzania yajitokeza sakata la matibabu ya Mdamu

Muktasari:

  • Nyota huyo wa zamani wa Mwadui, amefahamishwa wazi kwamba kwa sasa hataweza tena kucheza soka, kitu ambacho amekipokea kwa uchungu na kukubali hali halisi.

Inasikitisha, lakini ndio ukweli ulivyo. Gerald Mathias Mdamu aliyewahi kutamba katika soka kupitia timu kadhaa ikiwamo Polisi Tanzania, sasa atakuwa mtazamaji tu wa mchezo huo. Hii ni kutokana na taarifa aliyofahamishwa na daktari aliyemfanyia upasuaji wa kwanza baada ya ajali ya gari ya Julai, 2021.

Nyota huyo wa zamani wa Mwadui, amefahamishwa wazi kwamba kwa sasa hataweza tena kucheza soka, kitu ambacho amekipokea kwa uchungu na kukubali hali halisi.

Mdamu alikumbwa na ajali hiyo wakati basi la timu aliyokuwa akiitumikia wakati huo, Polisi Tanzania lilipoacha njia na kugonga mti na kusababisha kuvunjika miguu yote miwili, wakati wakitoka mazoezi mjini Moshi kujiandaa na mechi mbili za kufungia msimu wa 2020-2021.

Tangu apate ajali hiyo, mchezajio huyo alifanyiwa upasuaji na kuendelea kujiuguza kabla ya hivi karibuni Mwanaspoti kumtembelea nyumbani kwake kumjulia hali na kubainika bado anaishi katika hali ya mateso na maumivu kutokana na majeraha aliyoyapata ambapo wadau mbalimbali wamejitokeza kumsaidia.

Mmoja ya wadau walioshtushwa na hali ya Mdamu alikuwa ni daktari aliyemfanyia upasuaji kutoka Moi, Dk Kennedy Nchimbi ambaye aliomba mchezaji huyo aendee hoispitalini hapo ili kumfanyia uchunguzi kabla ya kumweleza ukweli kwamba hataweza tena kucheza soka.

Hata hivyo, mchezaji huyo ameikubali hali ya kuishi plani nyingine baada ya kushauriwa na daktari ya nini kifanyike, ili maisha yake mengine yaendelee, huku akuijulishwa pia anatakiwa kufanyiwa upasuaji mwingine ili kurekebisha tatizo lake la kutokwa na usaha katika majeraha aliyonayo.


WASIKIE POLISI TANZANIA FC

Katibu Mkuu wa Polisi Tanzania, ASP Michael Mtebene amesema kama taasisi watakaa na kuangalia namna nzuri ya kumsaidia mchezaji huyo, huku akiweka wazi pia wanaguswa kwa maana moja au nyingine kwa sababu alikuwa ni mchezaji wao.

"Tumeona kampeni mbalimbali ambazo zinaendelea na sisi kama taasisi tunaguswa kwa sababu alikuwa ni mchezaji wetu, hatujamtupa kama ambavyo wengi wao wanazungumza ila, wadau wa soka wanapaswa kutambua kila sekta ina taratibu zake," alisema Mtebene.

Mtebene aliongeza, Mdamu walikuwa wakimlipia kila kitu wakati akiwa na kikosi hicho, ingawa gharama za kiundeshaji kwa maana timu iliposhuka daraja ndipo wakasitisha utaratibu huo, ingawa haina maana kwamba hawawezi kumchangia kwa sasa.