Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pak Stars, Gymkhana zafunika daraja la tatu

STARS Pict

Muktasari:

  • KUPUNGUA kwa mvua jijini Dar es Salaam kumeamsha tena moto wa kriketi ambao umezileta ligi tatu tofauti katika viwanja vya Gymkhana, Leaders Club na Anadil Burhan,

KUPUNGUA kwa mvua jijini Dar es Salaam kumeamsha tena moto wa kriketi ambao umezileta ligi tatu tofauti katika viwanja vya Gymkhana, Leaders Club na Anadil Burhan,

Ligi ya TCA-Diwa kwa wanaume, Ligi ya kufuzu michuano ya Caravans na Ligi B ya TCA kwa wanaume ndizo zilizoipamba kriketi mwishoni mwa juma.

Timu zilizotoka kifua mbele ni pamoja na Pak Stars ambayo imeanza vyema michuano ya Ligi ya Diwa baada ya kuifunga timu ya Cricket Gunners kwa mikimbio 21 katika mchezo wa mizunguko 10 uliochezwa jijini mwishoni mwa juma.

Pak Stars ndiyo walioanza kubeti na kufanikiwa kutengenzeza mikimbio 101 huku wakipoteza wiketi 8 baada ya kumaliza mizunguko yote 10 ya mchezo huo.

Jitihada za vijana wa Cricket Gunners kuifukuzia mikimbio ya wapinzani wao ziligota kwenye mikimbio 70 baada ya kumaliza mizunguko yote 10 wakiwa wamepoteza wiketi 6 na hivyo kuwafanya Pak Stars kuondoka na ushindi wa mikimbio 31.

Ushindi wa Pak Stars ulichagizwa na Nisar Ahmed aliyetengeneza mikimbio 34 akisaidiwa na Muhammad Mudasser aliyeleta mikimbio 24 pamoja na Ayaz Mustafa aliyepiga mikimbio 15.

Katika mechi za kufuzu kucheza michuano ya Caravans, timu ya Gymkhana iliifunga Dar Indian Titans kwa wiketi 8 katika mechi iliyochezwa pia mwishoni mwa juma kwenye Uwanja wa Gymkhana.

Dar Indian Titans ndiyo walioanza kubeti na kufanikiwa kutengeneza mikimbio 82 baada ya wote kutolewa wakiwa wametumia mizunguko 18 kati ya 20 ya mchezo huo.

Haikuwa kazi ngumu kwa vijana wa Gymkhana kuzifikia alama za wapinzani wao na kushinda.

Wakitumia mizunguko 10 kati ya 20 ya mchezo huo, vijana wa Gymkhana walitengezea mikimbio 84 huku wakipoteza wiketi 2 tu na hivyo kushinda kwa wiketi 8.

Walioipaisha Gymkhana kwa upande wa wiketi ni Sai Surya, Nikila Nishanga na Dharmin Parmar  ambao walishinda wiketi 2 kila mmoja wakati Pankaj Vats    na Abdulrazak Mohamed Amiri walipata wiketi 1 kila mmoja.

Ligi 2 ya  TCA  ilishuhudiwa timu ya Patel Titans ikipata ushindi wa wiketi 6 dhidi ya Lions C katika mchezo wa mizunguko 20 uliopigwa pia jijini.