Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Coastal Union kung’oa chuma Kagera

Muktasari:

  • Coastal Union inapambana kuinasa saini ya beki wa Kagera Sugar, Mohammed Salum aende kuongeza nguvu kwenye kikosi chao.

WAKATI Kagera Sugar, ikijiuliza inarudije chini kucheza ligi ya Championship, baada ya kushuka daraja Coastal Union, inataka kuongeza maumivu kwenye kidonda ikimtaka beki wao wa kati.

Coastal Union inapambana kuinasa saini ya beki wa Kagera Sugar, Mohammed Salum aende kuongeza nguvu kwenye kikosi chao.

Taarifa kutoka ndani ya Coastal Union ni kwamba, beki huyo amependekezwa na makocha wa timu hiyo, baada ya kuonyesha ubora mzuri licha ya timu yake kushuka daraja.

Bosi mmoja kutoka ndani ya Coastal Union alisema, mazungumzo kati ya klabu yao na Salum yanaendelea ambapo kabla ya kuhamia Kagera Sugar.

Hata hivyo Coastal Union, itatakiwa kutumia msuli kumpata Mussa kwani mmoja wa viongozi waandamini wa Kagera Sugar ameweka wazi kwamba watambakisha kwavile wamepania kurudi. “Tunapambana pia kumpata Mussa yule beki wa Kagera Sugar, ni beki mzuri mpambanaji ingawa atatokea kikosi ambacho kimeshuka daraja. Tumekuwa tunamfuatilia kwa muda na tumeona anafaa kuja kuongeza nguvu, tunahitaji beki mwingine wa kati aje aongeze nguvu.”

Coastal Union ambayo inashika nafasi ya 10 katika ligi imecheza mechi 28 mpaka sasa,imeshinda saba,sare 10 na imepoteza 11,ikiwa na pointi 31.

Kagera iko nafasi ya 15.