Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Oljoro sasa yajishika na Yanga kashfa ya kupanga matokeo

Kikosi cha wachezaji cha JKT Oljoro.

Muktasari:

“Hivi kufungwa saba kuna ajabu gani hapo wakati Yanga iliwahi kumfunga Coastal Union tena Ligi Kuu mabao manane, nashangaa wanaozusha kuwa mchezo ulikuwa umenunuliwa, sasa Oljoro wana nini wasifungwe mabao 7,” alihoji Nalinga.

KATIBU Mkuu wa JKT Oljoro, Hussein Nalinga, ameshangazwa na taarifa zinazozagaa kila kukicha kuwa Oljoro wameuza mchezo wao dhidi ya Polisi Tabora ili hali wanafahamu kuwa kitendo hicho hakikubaliwi katika michezo.

“Hivi kufungwa saba kuna ajabu gani hapo wakati Yanga iliwahi kumfunga Coastal Union tena Ligi Kuu mabao manane, nashangaa wanaozusha kuwa mchezo ulikuwa umenunuliwa, sasa Oljoro wana nini wasifungwe mabao 7,” alihoji Nalinga.

Nalinga aliongeza kuwa kufungwa kwao kulitokana na uchovu wa safari ambayo ilikumbwa na matatizo baada ya gari walilotumia kusafiria kuharibika njiani nyakati za usiku na ikawapasa kukodisha usafiri mwingine hivyo wachezaji hawakupata muda wa kutosha wa kupumzika

“Kulikuwa hakuna figisu yoyote sisi tulichelewa kuondoka kwa sababu tulikuwa tunasubiri majibu ya barua yetu tuliyotuma TFF kupinga matokeo dhidi ya Geita na hatimaye Geita wakapewa Pointi tatu na mabao matatu na taarifa hiyo ilikuja kwa kuchelewa hivyo hatukuwa na jinsi kuondoka jioni ya Ijumaa” aliongeza kusema Nalinga

Hata hivyo aliongeza kwa kusema kuwa kuwepo kwa majeruhi wengi wa kikosi cha kwanza pia kilisababisha wao kupata kichapo hicho kinachozua maswali kila kukicha

“Kipa namba moja ni majeruhi hivyo ikabidi acheze Kipa namba mbili Shahibu Issa naye hakudumu baada ya kuumia ikabidi Kocha amchezeshe kipa namba tatu Oscar Ntanda ambaye hajawahi kucheza mchezo hata mmoja na akafungwa mabao 6,”alisema.

ARFA WAONA AIBU

Katibu Mkuu wa Chama cha soka Mkoa wa Arusha(ARFA), Adam Brown, amesema kuwa kitendo cha timu ya Soka ya JKT Oljoro ya jijini hapa iliyokuwa ikishiriki ligi daraja la kwanza (FDL) iliyomalizika wiki iliyopita cha kushutumiwa kupanga matokeo ni aibu kubwa.

Brown alisema kuwa hawezi kuamini kama Oljoro waliuza mchezo wao dhidi ya Polisi Tabora na kukubali kufungwa mabao 7-0 kwa kuwa Timu hiyo inafahamu kitendo hicho hakikubaliki.

“Siwezi kuwashutumu moja kwa moja Oljoro kuwa wamehusika acha tusubiri Chombo husika wafanye uchunguzi na kutoa maamuzi kulingana na ripoti za waamuzi waliochezesha na kusimamia mchezo huo,” alisema Brown.

Aliongeza kuwa Uongozi wa Oljoro haukupenda kushirikiana na Uongozi wowote wa soka mkoani hapa katika mambo yake na ndio maana wanajikuta mambo yao yakigonga mwamba kila wakati.

MACHUPA WA SIMBA ASHANGAA

“Soka yetu inasikitisha sana inapokwenda, leo watu wanajifanya wanashangaa matokeo ya Geita na Polisi Tabora ila haya madhara tusimlaumu mtu wakati kila siku watu wanalalamika kuhusu upangaji ila watu wanajitia hawaoni na wala hawajali,” alisema.

“Hatuna Uongozi imara na endelevu na soka yetu haiwezi kuendelea kwa kupanga matokeo, endeleeni kuwekeza kwenye kupanga matokeo, tunavifikiria vipi vizazi vyetu,tujitafakari.”

Straika huyo wa zamani wa Simba, ameandika hayo kwenye ukurasa wake wa Facebook.

KANUNI

Kanuni: 42 Udhibiti kwa Klabu

(7) Klabu itakayothibitika kupanga matokeo ya mchezo kitatozwa faini isiyopungua shilingi milioni kumi (Tsh10,000,000/-) na kuondolewa faida yoyote iliyoipata kutokana na kupanga huko matokeo ya mchezo husika.

(8) Iwapo klabu inashindwa kulipa faini iliyotozwa sambamba na kushushwa daraja haitaruhusiwa kushiriki Ligi katika ngazi ilipo.