Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nyota Tembo Warriors kutimkia Uturuki

Nyota Tembo Warriors kutimkia Uturuki

Dar es Salaam. Nyota wa timu ya taifa ya soka la walemavu 'Tembo Warriors', Frank Ngairo amepata nafasi  ya kwenda kufanya majaribio  nchini Uturuku katika moja ya klabu kubwa inayoshiriki ligi kuu ya soka kwa watu wenye ulemavu nchini humo.

Siku chache tu baada ya kutangazwa kua ni mchezaji wa bora wa mashindano ya Bara la Afrika ya soka kwa watu wenye ulemavu (CANAF) yaliofanyika hapa nchini na huku akiwa na mchango mkubwa wa kuipeleka Tanzania Kombe la Dunia ambapo aliifungia timu yake mabao 5.

Kiungo huyo maarufu kama 'Mbappe' aliliambia Mwananchi kuwa hakutarajia na wala hakua na mategemeo ya kwenda kucheza soka la kulipwa nje kwa wakati huu.

"Alinitafuta nahodha wa timu ya taifa ya Misri Mahmud Tawfik mara baada tu ya mashindano kufungwa kisha akaniaomba namba zangu za simu na akaniambia kuwa kocha wa klabu yake (Izmir) anahitaji kuzungumza na mimi"

"Siku iliyofuata kocha huyo alinitafuta na kuniuliza kama naweza kujiunga na klabu hiyo nami nikamjibu kuwa naweza pia nikwambia awataarifu uongozi wangu kuhusiana na suala hilo" alisema Ngairo
Mwananchi lilifanikiwa kumpata kocha wa klabu hiyo ya nchini Uturuki Uvren Uyanik ambapo alilithibitisha na kuweza wazi kuhitaji huduma ya Ngairo katika kikosi chao.

"Tulizipata habari zake kupitia kwa mchezaji wetu raia wa misri aliyeshiriki mashindano hayon na kumshuhudia na pia tuliweza kupata baadhi ya video fupi akiwa uwanjani na tukavutiwa naye"

"Lakini pia ni mchezaji mwenye umri mdogo tena mwenye kiwango kikubwa ambacho hapo baadae anaweza kua tishio na anaweza kuisadia timu yetu kuchukua mataji mbalimbali"alisema Uyanik.

Akizungumza na gazeti la Mwanachi Katibu wa Shirikisho la soka la walemavu nchini (TAFF) Moses Mabulla Alisema kuwa kwao ni hatua kubwa katika kuutangaza mchezo wa soka la walemavu hapa nchini huku akimtakia heri katika safari yake ya soka.

"Sina mashaka na kiwango pamoja na ubora wake kiwanjani hivyo nahuakika ataweza kufanya vizuri huko aendako na kikubwa zaidi ni sisi kuwa nyuma yake na kumpatia sapoti na kuahikikisha anafikia ndoto zake na kulitangaza taifa lake naamini atatuletea heshima kubwa"alisema Mabulla.

Klabu hiyo ya Izmiri BBSK inayoshiriki ligi kuu ya soka la walemavu nchini Uturuki ipo nafasi ya nne katika msimamo na inashikilia vikombe takribani kumi za ligi hiyo huku ikwa na makombe mbalimbali ya soka la walemavu nchini humo na barani Ulaya.