Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ntibonela Bukeng aongoza tena kutupia BDL

BDL Pict

Muktasari:

  • Idadi hiyo ya alama alizotupia mchezaji huyo ni kiashiria kwamba anakimbiza kwa kasi tuzo ya utupiaji katika mashindano hayo kwani wiki tatu zilizopita Bukenge aliongoza kwa pointi 124 akifuatiwa kwa karibu na Enerico Maengela anayekipiga ABC aliyefunga pointi 118.

NYOTA wa kikapu wa Savio, Mkongomani Ntibonela Bukeng anaendelea kuongoza kwa ufungaji katika Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL), akiwa keshatupia nyavuni pointi 213.

Idadi hiyo ya alama alizotupia mchezaji huyo ni kiashiria kwamba anakimbiza kwa kasi tuzo ya utupiaji katika mashindano hayo kwani wiki tatu zilizopita Bukenge aliongoza kwa pointi 124 akifuatiwa kwa karibu na Enerico Maengela anayekipiga ABC aliyefunga pointi 118.

Katika rekodi za sasa, Bukeng ambaye ni raia wa DR Congo amemwacha kwa mbali mchezaji mwenzake mwingine Godfrey Swai anayeshika nafasi ya pili akiwa na pointi 159, huku ile ya tatu inakamatiwa na Yasin  Shomari wa Mgulani JKT aliyefunga 142, ilhali Maengela wa ABC akishika nafasi ya nne na pointi 136.

Wachezaji wengine ni Jamel Marbuary Dar City aliyetupia pointi 135, Jonas Mushi (Stein Warriors 128), Jamal Hussein  (Mchenga Star 125), Sharom Ikendigwe (Dar City 120), Victor Michael (Vijana 114) na Junior Louissi mwenye pointi 113.

Eneo jingine ambalo limekuwa na ushindani mkali katika ligi hiyo ni lile la utupiaji la three point ambapo mbabe wao hadi sasa ni Ally Abdallah wa Dar City anayeongoza kwa kufunga eneo moja kwa pointi 20 akifuatiwa na Zadock Emmanuel wa Kurasini Heat aliyefunga three point 18 akilingana na Abdul Kakwaya (Vijana 18 pia), Jamel Marbuary (Dar City, Yasin Shomari (Mgulani), Peter Chacha (Mchenga Star) na Jonas Mushi (Stein Warriors) wote wakiwa wametupia 17 huku Mikado Ebengo (UDSM) na Hassan Kabanda (DB Oratory) wakifunga 16 na Oscar Mwituka wa Savio aliyefunga 15.

BD 01

TIMU TATU ZAKABANA WBDL

Mchuano mkali katika Ligi ya Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam upande wa wanawake (WBDL), uko kwa timu za Tausi Royals, Jeshi Stars na JKT Stars baada ya kufungana pointi sawa - 14, huku kila timu ikiwa imecheza michezo saba. Ligi hiyo ushindani umeongezeka tofauti na mwaka jana ambapo timu zilizokuwa katika nafasi za juu ziliachana kwa   pointi nyingi.

Ligi ya mwaka jana kuchezwa katika mizunguko miwili, msimu huu imeonyesha hadi kufikia michezo 28 DB Troncatti ilikuwa inaongoza kwa pointi 53, Tausi Royals 49 na Pazi Queens 47.

Takwimu za msimamo wa ligi ya WBDL zinaonyesha kwamba Tausi Royals inaongoza kwa pointi 14 ikifuatiwa na Jeshi Stars (14) JKT Stars (14), DB Troncatti (14), DB Lioness (13), Twalipo Queens (12), Polisi Stars (11), Pazi Queens (11), Vijana Queens (10) na Reel Dream (9).

BD 02

PAZI SASA MOTO BDL

Ushindi ilioupata Pazi dhidi Polisi wa pointi 90-40 katika BDL umeifanya ipande kutoka nafasi ya tano hadi ya pili.

Mchezo huo wa kiporo uliofanyika katika Uwanja wa Donbosco Upanga ulishuhudia timu hiyo ukiishusha ABC hadi nafasi ya tatu. Ligi hiyo inayochezwa kwa mzunguko mmoja, imeonyesha ushindani mkubwa kwa timu zote zinazoshiriki kutokana na viwango   vinavyoonyeshwa kwa timu shiriki.