Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nsajigwa, Bonny waosha Nepal

Shadrack Nsajigwa(wa kwanza kushoto mstari wa mbele) na Bonny (wa pili kutoka kushoto mstari wa nyuma) wakiwa kwenye kikosi cha Saraswoti.

Muktasari:

  • Wachezaji hao wote walijiunga kwa pamoja kwenye klabu hiyo katika msimu huu wa Ligi Kuu kimya kimya bila kutaka Watanzania wajue kinachoendelea.

WATANZANIA wanaocheza soka la kulipwa huko Nepal, Shadrack Nsajigwa, Godfrey Bonny na Pius Kisambale wameonekana kung’ara kutokana na kuiwezesha klabu yao ya Saraswoti Youth Club kupata matokeo mazuri katika mechi tano walizocheza.

Wachezaji hao wote walijiunga kwa pamoja kwenye klabu hiyo katika msimu huu wa Ligi Kuu kimya kimya bila kutaka Watanzania wajue kinachoendelea.

Nsajigwa kabla ya kwenda kucheza soka nchini humo, alikuwa Kocha Mkuu wa Lipuli FC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza, pia aliwahi kuwa nahodha wa Taifa Stars na Yanga ambayo ilimtema kwa madai kuwa umri umekwenda na kiwango kimeshuka.

Nsajigwa aliwahi kucheza pamoja na wachezaji Bonny na Kisambale katika klabu ya Yanga na Prisons ya Mbeya kuipa mataji tofauti ya ubingwa.

Kisambale kabla ya kwenda huko alikuwa akiichezea Coastal Union ikamtema. Saraswoti hadi sasa imeshinda mechi mbili, sare mbili huku ikifungwa moja pekee.