Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nimubona ni msuli bhana

Beki wa kulia, Emiry Nimubona.

Muktasari:

Katika mechi tano ambazo Simba imecheza, Nimubona amecheza dakika 45 pekee katika mechi dhidi ya Kagera Sugar iliyochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo Simba ilishinda mabao 3-1.

Wakati akijiandaa kupata shavu la kucheza dakika zote 90 kutokana na Kessy kuwa na kadi tatu za Nimubona anakumbana na balaa baada ya kuumia mfupa wa kidole cha mkono na hivyo kulikosa shavu hilo dhidi ya Mbeya City.

SIMBA iliamua kufunga safari mpaka nchi jiranji ya Burundi na kumsajili beki wa kulia, Emiry Nimubona. Haukuwa usajili wa kubahatisha na wala haukuwa na longolongo, kila kitu kilikuwa peupe kwa beki huyo kutua Msimbazi akitokea Vital’O.

Mabosi wa Simba waliotumwa Burundi waliridhishwa na kiwango chake na kuamua kufanya naye mazungumzo kabla ya kumsajili hasa baada ya mkataba wake na Vital’O kuelekea ukingoni.

Hata hivyo, tangu atue Simba, hajabahatika kucheza kwa muda mrefu kutokana na kiwango alichonacho, Hassan Kessy anayecheza naye katika nafasi hiyo ya beki wa kulia.

Katika mechi tano ambazo Simba imecheza, Nimubona amecheza dakika 45 pekee katika mechi dhidi ya Kagera Sugar iliyochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo Simba ilishinda mabao 3-1.

Wakati akijiandaa kupata shavu la kucheza dakika zote 90 kutokana na Kessy kuwa na kadi tatu za Nimubona anakumbana na balaa baada ya kuumia mfupa wa kidole cha mkono na hivyo kulikosa shavu hilo dhidi ya Mbeya City.

Katika mahojiano na Mwanaspoti, Nimubona amezungumza mambo mbalimbali kuhusiana na soka lake, Ligi Kuu Bara na mengineyo katika maisha ya soka.

Pesa nje nje

Nimubona anasema soka la Tanzania halina tofauti kubwa na soka la Burundi, tofauti pekee anayoiona ni juu ya maslahi kwamba Tanzania upatikanaji wa fedha kupitia soka ni rahisi kuliko Burundi.

“Burundi watu wanacheza mpira kwa sababu tu wanapenda ila hakuna masilahi yoyote ukilinganisha na hapa Tanzania, ndiyo maana unaweza kuona kama soka la Tanzania lipo juu kwa sababu watu wengi wanakuja kutafuta pesa kwa ajili ya maisha yao. Tofauti ni ndogo sana kimpira ukifanya uchunguzi Burundi ipo juu kwani kila mchezaji anacheza kwa kujituma ili apate sehemu nyingine ya kucheza na kujipatia kipato kikubwa,” anasema Nimubona.

Malengo

Anasema kabla ya kutua Simba alikuwa amefanya uchunguzi, aliambiwa mengi lakini aliona ni vyema ayashuhudie mwenyewe kuliko kusimuliwa ila anaamini hali si tofauti sana na alivyosimuliwa.

“Wakati tunakubaliana na Simba kuhusu mkataba tulizungumza mambo mengi, ukiachana na fedha za usajili, mshahara lakini pia niliwaomba wanitimizie suala la nyumba na kula, bado sijapata nyumba ila naamini watanitafutia kwani kuna hatua wamefikia ambayo ni nzuri na ni ya mafanikio.

“Unajua mchezaji akitimiziwa kila kitu, basi deni linabaki kwako ambaye unatakiwa kulipa yale uliyopewa kwa kuisadia timu ifanye vizuri kwenye mashindano, hivyo hata kwangu itakuwa hivyo, maana unapoomba utekelezewe jambo lako usifanye kama vita, sisi ni binadamu tunatakiwa kuelewana tu,” anasema.

Nafasi kikosini

Licha ya kutocheza mechi nyingi akiwa Simba, bado ana imani kubwa nafasi yake ndani ya kikosi cha Kerr ipo tena iko wazi. “Huwa inakatisha tamaa kukaa nje bila ya kucheza na inaumiza, ila inahitaji uvumilivu mkubwa hasa kama unaamini una uwezo wa kucheza.“Najiamini na ninajua nafasi yangu ipo wazi ndani ya Simba ni muda tu bado haujafika. Unapokuwa mchezaji wa kigeni unatakiwa kuwa na vitu vya ziada kuhakikisha unamzidi yule uliyemkuta na kumwondoa si kwa mara moja tu, ninachokifanya ni kuongeza juhudi na kufanya mambo ambayo yeye hana, kikubwa waniamini wanipe mechi nyingi ili waone kiwango changu kikoje,” anasema

Ubora wa Kessy

Anasema Kessy ni mchezaji mzuri na kitu pekee ambacho Kessy kinaweza kumbeba zaidi ni uzawa, huku akidai kuwa uchezaji wa Kessy na yeye una tofauti kubwa sana ambapo Kessy kuna vitu hana.

“Nina kazi kubwa ya kufanya ingawa najua nitacheza hata kama nitachukuwa muda mrefu. Nimemzidi Kessy baadhi ya vitu kwani naweza kupiga krosi zinazozaa matunda, kukaba na kuzuia kwa wakati mmoja ndiyo maana nasema nafasi yangu ipo.”

Maisha ya Simba

“Simba ni timu kubwa, ina mashabiki wengi tofauti na Yanga, hivyo maisha ni mazuri kwani wanaonyesha kujali hasa pale unapowapelekea tatizo lako. Unajua hakuna sehemu ambayo haina matatizo, hata kwenye familia zetu kuna matatizo, kikubwa ni kukaa na kuelewana ikiwa ni pamoja na kutatua matatizo yetu kwa amani,” anasema.

Akiwazungumzia baadhi ya nyota wa Burundi wanaocheza nchini, Nimubona alisema anafurahi kuishi Tanzania nchi ambayo amekutana na raia wenzake wa Burundi ambao ni Amissi Tambwe wa Yanga na Dider Kavumbagu wa Azam huku akitoa neno hasa kwa Kavumbagu anayeonekana kukataa tamaa kutokana kuwekwa benchi na Kocha Stewart Hall.

Vurugu Burundi

“Unajua kabla ya haya machafuko ya kisiasa kutokea nchini kwetu, watu walikuwa wanapenda sana mpira na kulikuwa na ushindani mkubwa, hivi sasa hakuna mtu anayeweza kwenda uwanjani kushuhudia mechi wakati muda wowote risasi zinapigwa, hivyo hata ule ushindani umepungua.

“Hapa tunaona ushindani mkubwa hasa Simba na Yanga zinapocheza, hiyo hata Burundi ilikuwepo ila sasa hivi hakuna tena labda mpaka machafuko hayo yamalizike kabisa.”

Akizungumzia familia yake, Nimubona anasema; “Nina mpango wa kuihamisha familia yangu kuja Tanzania kutokana na machafuko hayo, nakosa amani kusikia kila siku risasi zimepigwa, naweza kupoteza familia wakati nikiwa huku, najua itaniathiri kisaikolojia ambapo nitashindwa kucheza vizuri kama familia itaendelea kuishi Burundi.

“Pia sioni sababu ya kutuma fedha za matumizi wakati familia yangu iko kwenye nchi yenye vita, nitawaomba viongozi wangu wanisaidie kunipatia nyumba haraka ili nikienda mapumziko nirudi nao,” anasema Nimubona akiwa na mpango wa kumleta mke, mtoto wa kiume mwenye miaka sita pamoja na mwingine anayetarajia kumpata mwezi ujao.

Ubigwa Simba

“Simba tuna nafasi ya kutwaa ubingwa inagwa huwa tunapata ushindi wa mabao machache tofauti na wenzetu Yanga. Kinachowasaidia Yanga kupata mabao mengi ni kutokana na kuwa na wachezajai wengi wazoefu wanaotoka ndani na nje ya nchi.

“Timu yetu ina vijana wengi ingawa wana uwezo na kasi, kikubwa ni kuongeza juhudi ili kuipita Yanga naamini tuna nafasi hiyo ya kutwaa ubingwa wa ligi.”