Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ngorongoro ina dakika 90 za uamuzi AFCON-U20

NGORONGORO Pict
NGORONGORO Pict

Muktasari:

  • Ushindi utaifanya Tanzania kufikisha pointi tatu na kusikikilizia matokeo ya mechi ya mwisho dhidi ya wenyeji ili kuona kama itatoboa hata kupitia mshindwa bora (best Looser) ikishika nagasi ya tatu ya kundi ili kuungana na washindi wawili wa kila wa makundi matatu kutinga robo fainali.

BAADA ya timu ya taifa ya vijana, Ngorongoro Heroes kupoteza mechi mbili za awali za Kundi A katika vita ya kuwania ubingwa wa Afrika (AFCON-U20), kwa sasa timu hiuo ina dakika 90 za kufufua tumaini la kuvuka hatua hiyo kwenda hatua inayofuata kusaka tiketi ya fainali za Kombe la Dunia 2025.

Ngorongoro imesaliwa na mechi mbili, ikiwamo ya kesho Jumanne dhidi ya Zambia na ile ya Mei 9 itakapovaana na wenyeji wa fainali hizo, Misri, lakini pambano la kesho ndilo lililoshikilia hatma ya Tanzania kuendelea kuwepo michuanoni au kuaga rasmi. Kama itapoteza mbele ya Zambia itakuwa na maana timu hiyo imeaga rasmi na itaenda kukutana na Misri ili kukamilisha ratiba tu na matokeo ya ushindi hayataisaidia kuwavuka kutoka katika Kundi hilo kwenda robo fainali.

Mechi hiyo ya Ngorongoro dhidi ya Zambia itapigwa kesho kwenye Uwanja wa Suez Canal, Ismailia na itahitaji ushindi pekee ili kufufua tumaini, baada ya awali kuanza vibaya michuano kwa kupoteza mechi mbili za awali kwa kulala 1-0 kila moja mbele ya Afrika Kusini na Sierra Leone.

Tanzania inaburuza mkia ikiwa ndio pekee isiyokuwa na pointi yoyote licha ya kucheza mechi mbili, wakati Zambia inayokutana nayo ipo juu yake nafasi ya nne ikiwa na alama mbili ilizotokana na sare ilizopata dhidi ya Sierra Leone na Misri. Siera Leone ndio vinata wa kundi hilo ikiwa na pointi saba, ikifuatiwa na Misri yenye nne zikiwa zimecheza mechi tatu kila moja, huku Afrika Kusini ikiwa ya tatu na alama zao tatu ikicheza mechi mbili kama ilivyo kwa Zambia na Tanzania.

Ushindi utaifanya Tanzania kufikisha pointi tatu na kusikikilizia matokeo ya mechi ya mwisho dhidi ya wenyeji ili kuona kama itatoboa hata kupitia mshindwa bora (best Looser) ikishika nagasi ya tatu ya kundi ili kuungana na washindi wawili wa kila wa makundi matatu kutinga robo fainali.

Hata hivyo, licha ya kuhitaji ushindi, lakini Ngorongoro itakuwa inaiombea mabaya Afrika Kusini itakayovaana na Sierra Leone ili ipoteze, kwani Wasauzi wakishinda watafikisha pointi sita na kujiweka pazuri kuibania Tanzania isiende kwa matokeo ya wenyewe kwa wenyewe kama watafunga pointi.

Wasauzi nao watasaliwa na mechi nyingine moja ya kumalizia makundi dhidi ya Zambia siku ambayo Tanzania itakuwa inamenyana na wenyeji, Misri.

Licha ya ugumu wa mechi hizo zilizasalia baadhi ya wachezaji wa Ngorongoro wamesema wamejipanga kupambana, licha ya kuchemsha mechi mbili zilizopita.

Akizungumza na Mwanaspoti, mshambuliaji wa timu hiyo, Morice Sichone alisema matumaini ya kucheza fainali hizo yapo kwa Zambia kama wachezaji wanajua umuhimu wa mchezo huo.

"Tumekuwa na mechi nzuri lakini shida inaonekana hatujapata maelewano kwenye eneo la ushambuliaji na kocha amekuwa akisisitiza sana, tunajua safari ya kurudi Dar itakuwa dhidi ya Zambia," alisema Sichone na kuongeza

"Nimecheza Zambia karibu nusu msimu sasa baadhi ya wachezaji nawafahamu na hata benchi la ufundi naamini itasaidia kwa kiasi fulani."