Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nne Mbeya City zampa heshima Malale

MALALE Pict

Muktasari:

  • Malale aliyejiunga na kikosi hicho Machi 31, 2025 akichukua nafasi ya Salum Mayanga aliyetua Mashujaa FC, ameweka rekodi hiyo akiiongoza katika mechi nne za Championship, akianza na sare ya bao 1-1, dhidi ya Biashara United, Aprili 12, 2025.

KOCHA wa Mbeya City, Malale Hamsini ameandika rekodi nyingine kwa kuipandisha timu Ligi Kuu Bara msimu ujao, ikiwa ni kwa mara ya pili tangu afanye hivyo msimu wa 2022-2023, akiwa na kikosi cha maafande wa JKT Tanzania.

Malale aliyejiunga na kikosi hicho Machi 31, 2025 akichukua nafasi ya Salum Mayanga aliyetua Mashujaa FC, ameweka rekodi hiyo akiiongoza katika mechi nne za Championship, akianza na sare ya bao 1-1, dhidi ya Biashara United, Aprili 12, 2025.

Mechi nyingine ni ushindi wa mabao 4-2, dhidi ya Polisi Tanzania, Aprili 18, 2025, akaichapa Geita Gold 3-2, Aprili 26, 2025, kisha 5-0, mbele ya Cosmopolitan Mei 1, 2025 na kukata rasmi tiketi ya kucheza Ligi Kuu sambamba na Mtibwa Sugar.

Ushindi na Cosmopolitan ukaifanya kurejea tena Ligi Kuu Bara msimu ujao, baada ya kushuka daraja msimu wa 2022-2023, ikifikisha pointi zake 65, akishinda mechi 19, sare minane na kupoteza miwili, ikifunga mabao 63 na kuruhusu 26.

Akizungumza na Mwanaspoti, Malale alisema siri kubwa ni kutokana na ushirikiano mkubwa alioupata kuanzia kwa viongozi, wachezaji na mashabiki wa kikosi hicho, ambao ndio waliochangia kutimiza malengo waliyojiwekea tangu msimu huu umeanza.