Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mastaa hawa kuamua dabi

DABI Pict

Muktasari:

  • Timu zote ziko nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa Ligi ya Wanawake unaotetewa na Simba.

ZIMESALIA siku mbili kabla ya kushuhudia mtanange wa Dabi ya Dar es Salaam kati ya JKT Queens na Simba Queens kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo jumatano hii.

Timu zote ziko nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa Ligi ya Wanawake unaotetewa na Simba.

JKT iko kileleni na pointi 38 tofauti ya pointi moja na Simba iliyopo nafasi ya pili yenye 37.

Sasa katika dabi hiyo, Mwanaspoti limekuandikia dondoo za mastaa wanaoweza kuamua mechi hiyo muhimu kwa pande zote mbili.


Stumai, Winifrida (JKT)

Mshambuliaji, Stumai Abdallah ana nafasi kubwa ya kuisaidia JKT kuondoka na ushindi kutokana na mwenendo wake wa kufunga mabao akiwa ndiyeo kinara wa wafungaji akipachika 26.

Mwingine ni Winifrida Gerald mwenye mabao 10, winga huyo amekuwa nyota hatari anapokutana na mabeki wa Simba na Yanga na kusababisha penati kutokana na machachari yake ndani ya boksi la mpinzani.


Shikangwa, Wambui (Simba)

Kwa upande wa Simba, Jentrix Shikangwa ni miongoni mwa wachezaji hatari anapokuwa na mpira na ndiye kinara wa timu hiyo akifunga mabao 19.

Winga Elizabeth Wambui mwenye mabao saba kwenye mchezo uliopita alifunga bao moja kwenye sare ya 1-1 licha ya kutoimbwa sana lakini kasi yake, nguvu zinaweza kuwa na faida kwa Simba kama mabeki wa timu pinzani hawatakuwa makini nae.