Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ngailo amvutia kocha wake mazoezini

STAA wa Timu ya taifa ya walemavu Tembo Warriors, Frankcasian Ngailo 'Mbappe' ameanza kuonyesha makali yake hiyo jana katika uwanja wa mazoezini akiwa na Timu yake mpya Izimir BBSK ya nchini Uturuki.

Nyota huyo licha ya kuwa ilikua ni siku yake ya Kwanza akiwa na Timu hiyo haikua sababu ya yeye kushindwa kuonyesha kiwango chake jambo ambalo limemfanya kocha wake kumkubali.

Ngailo anasema kuwa kwake changamoto inayomkabili wakati huu ni ya nje ya uwanja akiitaja kuwa ni hali ya hewa ya mji wa Izimir ingawa anaamini kuwa ni jambo la muda tu kwani ataizoea.

"Hali ya hewa ya Huku ni tofauti na ya nyumbani muda mwingi ni baridi tu ingawa hata kule kwetu Ludewa kuna baridi lakini sio Kama nililolikuta Izimir" anaendelea na kusema;

"Namshukuru Mungu nimeanza kufanya mazoezi na wenzangu na siku ya Kwanza ilikua siku nzuri kwangu kwani niliweza kupata nafasi ya kuwatambua wachezaji wenzangu" anasema Ngailo akiwa nchini Uturuki.

Mwanaspoti lilifanikiwa kumpata kocha wa klabu hiyo ya nchini Uturuki Uvren Uyanik ambapo alilithibitisha kuwa nyota huyo na kusema alifika salama na tayari ameshaanza mazoezi na wenzake.

"Najua kuwa siku za hapa mwanzoni mazingira ya Izimir yatakua changamoto kwake lakini licha ya hivyo bado ameonyesha kiwango chake siku ya Kwanza katika uwanja wa mazoezi hivyo ninatarajia kuona mengi kutoka kwake" anasema Uyanik.

Nyota huyo wa Tembo warriors aliwasili Uturuki Jumanne saa sita mchana akitokea Tanzania saa 12 alfajiri  na shirika la ndege la Turkish Airlines.