Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Namungo yarahisishiwa kazi CAF

NDIO hivyo tena! Shirikisho la Soka Africa (CAF), limeamua michezo yote miwili ya Kombe la Shirikisho baina ya Namungo na CD Agosto ipigwe nchini Tanzania.
CAF imefikia uamuzi huo baada ya siku chache Namungo wakiwa Angola walikumbana na sintofahamu iliyopelekea mchezo huo kutopigwa kwa madai ya nyota wa Namungo kuwa na maambuziki wa virusi vya corona.
Taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) leo Februari 17, 2020 imeeleza CAF, wamefikia hatua hiyo baada ya kamati ya mashindano ya CAF kubaini sio Namungo wala Agosto waliokwamisha mchezo huo.


Baada ya wachezaji wa Namungo kukutwa na virusi hivyo walishindwa kucheza mchezo huo uliokuwa umepangwa kupigwa Februari 14 Nchini Angola na kulazimika kurejea nchini.
"Uamuzi huo umefanywa baada ya kamati ya CAF ya mashindano hayo kubaini kuwa sio Agosto wala Namungo iliyohusika moja kwa moja kukwamisha mechi ya kwanza hivyo mechi zote mbili zitachezwa angalau ndani ya saa 72 na zimechezwa kufikia februari 26 mwaka huu," imeeleza taarifa hiyo.


Kutokana na taarifa hiyo Agosto licha ya kucheza Tanzania mechi zote mbili, mchezo wa kwanza itawajibika katika maandalizi yote ikiwemo gharama za maofisa wa mechi hiyo.
"Kwa vile makundi ya kombe la shirikisho yatapangwa Februari 22 mshindi wa jumla baada ya mechi hizo mbili hatazingatiwa katika viwango (Non Ranked) wakati wa upangaji,".
Wachezaji watatu wa Namungo Lucas Kikoti, Fred Tangalu pamoja na Khamis Faki walibainika kuwa na maambukizi ya corona pamoja na Mtendaji wao Mkuu Omary Kaaya waliopelekea timu hiyo kuzuiliwa na kuwekwa karantini.