Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Namungo wakutana na figisu za hatari Angola

UNAWEZA kusema ni figisu figisu za soka la ukanda wa Afrika zilizoikumba timu ya Namungo inayowakilisha nchi katika michuano ya Kombe la Shirikisho baada ya nyota wao mahiri na tegemeo kuwekwa karantini.
Namungo imekumbana na sintofahamu hiyo baada ya kufika Uwanja wa ndege Nchini Angola ambapo kesho Februari 13 wanatarajiwa kumenyana na wapinzani wao Primeiro De Agosto.

Msafara wa Namungo wamejikuta wakikwama uwanjani hapo kwa madai ya baadhi ya wachezaji kupimwa na kukutwa na maambukizi ya virusi vya Covid 19.
Mwanaspoti imefanya mawasiliano na mmoja wa viongozi katika msafara huo, Ibrahim Mohamed ambaye amekiri kuzuiliwa kwa msafara huo uwanja wa ndege.
Ibrahim amesema katika msafara wao nyota wao watatu Lucas Kikoti, Fred Tangalu pamoja na Khamis Faki wamewekwa eneo tofauti na wao kwa madai ya kuonekana wana virusi hivyo sambamba na Mtendaji Mkuu wa klabu ya Namungo, Omary Kaaya.
"Ni kweli tumezuiliwa uwanja wa ndege, kwa muda ila kwa sasa hivi tumepelekwa nje ya mji kabisa, huku wenzetu wanne wao wakipelekwa sehemu nyingine hatujui wako wapi ila hatuko nao,"
Amesema kwa sasa wanaendelea kuwasiliana na chama cha soka nchini humo ili kujua hatima yao kwa kuwa mchezo wao unatarajiwa kuchezwa kesho.
"Tunawasiliana nao ili tujue nini kinafuata, hapa tuna ubalozi wa heshima alikuja uwanja wa ndege na kuondoka, tunawasiliana na CAF na tumewaeleza juu ya hili tunaendelea kusubiri," amasema Ibrahim.


KAULI YA WIZARA
Mkurugenzi wa Wizara yenye dhamana na michezo hapa Nchini Yusuph Singo amesema, wao kama Serikali wanajitahidi kwa ukaribu kuwasiliana na ubalozi wa Tanzania Nchini humo ili kulitatua suala hilo.
"Hatuko kimya nasisi kama Serikali tumeshituka na kushangazwa na hilo lakini tunalifanyia kazi tunawasiliana na wenzetu walioko huko,"
Namungo iliyondoka Nchini Tanzania jana saa moja usiku kuelekea Nchini humo na kujikuta katika wakati mgumu baada ya kukumbana na msukosuko huo na hasa ikizingatiwa ni mara ya kwanza kupata uwakilishi huu.