Namba hazisemi uongo, vita ya kiatu ni moto

LONDON, ENGLAND.MBIO ya Kiatu Dhahabu cha kwenye Ligi Kuu England inazidi kunoga.

Msimu mpya wa Ligi Kuu England, 2020/21 umeanza kwa staili matata kabisa huku mabao yakifungwa karibu kila kona.

Kwa ujumla wake, hadi ligi hiyo inasimama kupisha mechi za kimataifa, tayari yalikuwa yamefungwa mabao 144 katika mechi 38, ikiwa ni mabao 40 zaidi ya ligi hiyo ilipokuwa kwenye hatua kama hii kwa msimu uliopita.

Hata hivyo, tayari vita ya kusaka Kiatu cha Dhahabu imeanza kuonyesha taswira mambo yatakavyokuwa kwenye mchakamchaka huo wa Ligi Kuu England. Msimu uliopita, straika wa Leicester City, Jamie Vardy alifunga mabao 23 na kubeba kiatu hicho, akiwazidi kwa tofauti ya bao moja tu, straika wa Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang na Danny Ings wa Southampton waliofunga mara 22 kila mmoja.

Wakati huo huo, fundi wa mpira wa Manchester City, Kevin De Bruyne alipiga asisti 20 huku mchezaji mwenzake wa huko Etihad, Ederson alinyakua tuzo ya Golden Glove baada ya kudaka mechi 16 za ligi bila ya kuruhusu mpira kutinga kwenye wavu wake.

Na sasa, ligi ikiwa inaendelea, masupastaa wa Ligi Kuu England wameshaanza kuonyesha moto wao katika vita ya kusaka tuzo hizo binafsi na mambo ya uwanjani si haba, namba hazidanganyi