Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nabi amuacha Mayele, Mgunda ajilipua

Kwa Yanga hii mshaumia...Mayele amaliza utata

Ikiwa imesalia dakika chache kuanza kwa mchezo kati ya Yanga dhidi ya Coastal Union dhidi ya Yanga, Kocha Nabi amefanya mabadiliko ya kumuanzisha Heritier Makambo huku Mayele akisugua benchi.

Kikosi kinachoanza golini yuko Mshery, Djuma, Kibwana, Yanick,Nondo, Feisal, Aucho, Morrison, Moloko, Aziz Ki na Makambo huku benchi wakiwa ni Mayele, Farid, Ambundo, Lomalisa, Job, Bigirimana na Bacca.

Kikosi hicho inaweza kuwa ni surprise kwa mshabiki wa timu hiyo ambayo walikuwa na matumaini makubwa kwamba nyota wao Fiston Mayele na wengine kama Job na Lomalisa pengine wangeanza.

Katika mchezo wa leo kocha wa Coastal Union, Juma Mgunda ameonekana kufanya mabadiliko kadhaa kuhakikisha anaizuia Yanga na kuweza kuibuka na ushindi ambayo ndio malengo yao makubwa.

Kikosi cha Wagosi kinachoanza golini kuna  Mahamud Mroivili, akilindwa na Nimubona Emery, Miraji Hassan, Khatibu Ally, Lameck Elias, Mtenje Albano, Vicent Abubakary, Betrand Kunfor, Maabad Maulid,Greyson Gerald na Moubarack Amza.

 Wachezaji wa akiba ni Mohamed Hussein,Omary Iddi, Jackson Shiga, Joseph Mziwa, Gustavo Simon, Pembele Riguen, Hamadi Majimengi, William Kisingi na Optatus Lupekenya.

Mchezo huo unatazamiwa kuwa mgumu kutokana na ubora wa timu zote,Yanga wakihitaji kuendelea kuonyesha ubabe dhidi ya Coastal huku Wagosi hao wakitaka kulipa kisasi.

Mara ya mwisho timu hizo kukutana katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha,ilikuwa ni Julai 3 mwaka huu kwenye fainali ya kombe la Azam Sports (ASFC),timu hizo zikitoka sare ya 3-3 ndani ya dakika 120 huku Yanga ikishinda kwenye penati.