Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nabi aanza na wapya nane

Muktasari:

  • Yanga wanacheza mchezo huu wakiwa wamejihakikishia nafasi ya pili ambayo ni tiketi ya kucheza ligi ya mabingwa Afrika.

KOCHA Nassredine El Nabi wa Yanga, leo kwenye mchezo dhidi ya Dodoma Jiji,  amewaanzisha nyota wake wapya nane ambao hawakuanza mchezo iliyopita.

Katika mchezo uliopita ambao Yanga ilishinda mabao 2-0 dhidi ya Ihefu, wachezaji nane walioanza akiwemo mfungaji wa mabao yote mawili, Feisal Salum, wamewekwa benchi.

Ukiwa ni mchezo wa kukamilisha ratiba ya ligi kuu, inayotarajiwa kukamilika leo kwa timu zote kucheza jumla ya mechi 34.

Kocha Nabi, amewaanzisha kwa pamoja leo wachezaji nane ambao kati yao wamekuwa nadra kucheza kwenye mechi za timu hiyo msimu huu unaoishia.

Kipa Ramadhan Kabwili, huu utakuwa mchezo wake wa kwanza msimu huu, akianza badala ya Farouk Shikhalo, wakati Paul Godfrey, amekuwa mchezaji wa benchi zaidi msimu huu, nafasi yake ikichezwa na Kibwana Shomary.

Lamine Moro, ambaye tangu aliporudishwa Dar es salaam, kabla ya mchezo wa timu hiyo ugenini dhidi ya Namungo, hatimaye leo anacheza mchezo huu akiwa kama nahodha.

Kiungo Said Juma, ambaye naye amekuwa mchezaji wa benchi kwa mida mrefu, anacheza nafasi iliyozoeleka kuchezwa na Zawadi Mauya, tangu Nabi aanze kuionoa Yanga.

Deus Kaseke, Ditram Nchimbi, Wazir Junior na Saido Ntibazonkiza, kwa pamoja wameanza mchezo huu, japo wamekuwa wakipata nafasi ya kuingia kwenye mechi nyingi msimu huu.

Wachezaji waliokuwa wameanza kikosi cha kwanza kwenye mchezo wa ushindi dhidi ya Ihefu, walioanza na leo ni Adeyum Saleh, Bakary Mwamnyeto na Farid Mussa.