Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mzimbabwe mwili nyumba, mpira mwingi

Muktasari:

Akimzungumzia, Ngoma ambaye amekuwa gumzo Simba kutokana na namna anavyowatesa uwanjani kila wanapokutana, ambapo katika mechi ya mwisho waliyofungwa 2-0, ndiyo ilimletea matatizo beki wa kulia, Hassan Ramadhani Kessy ambaye sasa amejiunga na Yanga pamoja na Abdi Banda kuonyeshwa kadi nyekundu kwa sababu yake.

KOCHA Mkuu wa Simba, Mcameroon Joseph Omog amesema, Mzimbabwe Method Mwanjali ni beki wa kati na atamchezesha nafasi hiyo kama atakuwa naye kikosini, lakini beki huyo mwenye nguvu, akawatoa hofu mashabiki wa kikosi hicho juu ya Mzimbabwe wa Yanga, Donald Ngoma.

Mwanjali alisema Ngoma na ujanja wake wote anaijua vema shughuli yake uwanjani hivyo Wana Msimbazi hawana haja ya kuwa na presha yoyote msimu huu, ili mradi yeye yupo kikosini.

Beki huyo alisema mbali na Ngoma kumtambua vizuri, naye anamjua vyema straika huyo ambaye amekuwa akisumbua nchini tangu alipotua Jangwani akitokea FC Platinum ambapo katika mechi za watani msimu uliopita aliiumiza Simba nje ndani.

Ila akatoa angalizo, licha ya kumfahamu ili wafanikiwe lazima wawe na umoja kwani peke yake ni ngumu kufanikisha, wanachotakiwa ni kufanya kazi kwa pamoja na ushirikiano.

Mwanjali ambaye Omog amekuwa akimchezesha beki ya kati na kwa nyakati tofauti akimpanga na Novatus Lufunga, lakini zaidi na  Juuko Murshid raia wa Uganda. Katika mazungumzo na Mwanaspoti, Mwanjali alisema: “Nimefurahi kuja Simba timu nzuri, kuhusu maandalizi ni kama hivi, tunafanya kazi pamoja ili kutengeneza muunganiko mzuri na timu imara.”

Akimzungumzia, Ngoma ambaye amekuwa gumzo Simba kutokana na namna anavyowatesa uwanjani kila wanapokutana, ambapo katika mechi ya mwisho waliyofungwa 2-0, ndiyo ilimletea matatizo beki wa kulia, Hassan Ramadhani Kessy ambaye sasa amejiunga na Yanga pamoja na Abdi Banda kuonyeshwa kadi nyekundu kwa sababu yake.

Mwanjali alisema: “Ngoma Mzimbabwe mwenzangu ni mchezaji mzuri. Namjua na yeye ananijua vizuri sana, kazi yangu uwanjani na kwa kila kitu hivyo hakuna shida. Lakini pamoja na uwezo wangu, ili tufanikiwe  lazima tuwe na ushirikiano,  tukifanya kazi pamoja kila mtu akajua majukumu yake, hakuna kitakachoharibika,”alisema Mwanjali ambaye siyo mzungumzaji sana, zaidi kwake ni vitendo.

MWANJALI MAZOEZINI

Mwanjali ameonyesha uwezo wa juu na kukubalika na wachezaji wazawa ambao hawakutaka kutajwa majina, walisema: “Yule jamaa ni bonge la mchezaji na ni beki.”

Mwanaspoti imemshuhudia Mwanjali akichezeshwa nafasi ya beki wa kati, ana uwezo wa kucheza mipira ya chini, Ya juu, kukaba na kuchezesha timu, kwa haraka haraka wana ufanano na Muivory Coast wa Azam FC, Serge Wawa.

Hata hivyo, Omog amesema: “Sitaki kumzungumzia tena Mzimbabwe, subiri kauli rasmi ya uongozi. Mwenyewe umemwona mazoezi kwa kila kitu kazi kwako. Kuhusu nafasi na ubora wake kwenye uchezaji, ni mzuri kwenye beki ya kati ingawa ana uwezo wa kucheza nafasi nyingi za ulinzi ikiwemo ya kiungo mkabaji,”alisema Omog.

Mwanjali ni kati ya wachezaji wanne wa kigeni  wanaojaribiwa na Omog mkoani Morogoro, wengine ni Wacongo, Besala Bokungu na Moussa Ndusha na Muivory Coast Blagnon Frederick hata hivyo, Simba ilitegemea kuwapokea wachezaji wengine wa kigeni kutoka Ghana na Burundi.

ASUKA KOMBINESHENI

MAZOEZI ya Simba yamepamba moto na kuanzia jana Jumatatu, ni ufundi tu, kocha mkuu wa kikosi hicho, Mcameroon Joseph Omog na msaidizi wake, Jackson Mayanja raia wa Uganda wamekuwa na kazi ya kusuka kombinesheni kwa mifumo tofauti ya uchezaji.

Katika mazoezi hayo ya asubuhi ambayo yalikuwa ni kucheza tu, aligawa vikosi viwili, lakini akawa anavifanyia mabadiliko ya mara kwa mara ili kupata kombinesheni anayoitaka.

Kikosi cha kwanza, kilikuwa na kipa Muivory Coast Vincent Angban, Hamad Juma, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, beki ya kati alicheza, Mzimbabwe Method Mwanjali na Juuko Murshid raia wa Uganda, Said Ndemla na Mwinyi Kazimoto walicheza kiungo, Mdhamiru Yassin na Awadh Juma walicheza winga huku, Muivory Coast Blagnon Frederick na Mussa Mgosi wakicheza mastraika. Kikosi cha pili; kipa, Dennis Richard, mabeki wa pembeni, Malika Ndeule na Abdi Banda, wa kati  Mkongo Besala Bokungu na Novatus Lufunga, Mohamed Ibrahim na Peter Mwalyanzi walicheza kiungo, mawinga  Jamal Mnyate na Shiza Kichuya, wakati mastraika  ni  Ibrahim Ajib na Danny Lyanga.

Baada ya muda akawabadilisha vikosi kwa washambuliaji, Ajib na Muivory Coast, mabeki, Hamad na Kelvin Faru, Juuko na Nova, kiungo Mwalyanzi na Ndemla, Mohamed na Mdhamiru.

Katika mechi hizo ushindani ulikuwa wa juu kila mmoja akitafuta namba.

Baada ya hapo, Omog aliwanoa namna ya kufunga kupitia mipira ya pembeni kwa krosi. Mabeki wa pembeni ndiyo waliokuwa wapigaji wakati washambuliaji, mabeki wa kati na viungo kazi yao ilikuwa kufunga tu.

Staili ilivyokuwa, wachezaji hao wa pembeni  waliokuwa kushoto na kulia, walitoka wawili wakipasiana na kupiga krosi kati ambako pia walitoka wachezaji wawili waliOtakiwa kufunga. Omog alisema, lengo la mazoezi hayo ni kutengeneza timu yenye muungano:

“Ni kutengeneza timu yenye kufanya kazi pamoja na hapo ni namna ya kufunga.”