Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwakinyo afichua mipango ya kurudiana na Smith

Siku tatu baada ya kuchapwa na Liam Smith kwa Technical Knock Out (TKO), bondia Hassan Mwakinyo amefichua mipango ya pambano la marudiano.

Amesema amezungumza na promota wa pambano hilo nchini Uingereza na mabondia hao watarudiana Januari mwakani, nchini humo lakini kwenye mji tofauti.

"Halitachezwa tena kwenye mji wa Liverpool, makubaliano ni kwamba litafanyika Uingereza, lakini kwenye mji mwingine tofauti na Liverpool," amesema Mwakinyo leo alipokuwa akizungumza na Mwananchi Digital.

Mwakinyo usiku wa kuamkia Jumapili iliyopita alipigwa ma Smith kwa TKO ya raundi ya nne, pambano lililokuwa la raundi 12 la uzani wa super welter lililoacha maswali kwa mashabiki kwa namna ambavyo bondia huyo namba moja nchini aliacha akiwa anaongoza.

Katika pambano hilo, Mwakinyo alipiga magoti mara mbili raundi ya nne na kusalimu amri, licha ya kwamba raundi ya pili alimshambulia mfululizo mpinzani wake na bondia namba sita wa dunia na namba moja nchini Uingereza.

Japo alijitetea kwamba alipata maumivu ya enka, hivyo hakuweza kuendelea nalo na kuomba pambano la maruadiano ambalo leo amesema liko kwenye maandalizi lichezwe Januari mwakani.

"Sitakuwa na pambano jingine kwa sasa hadi nitakaporudiana na Smith mwezi Januari," amesema bondia huyo anayekamata namba moja nchini na wa 40 duniani.

Amesema keshokutwa Jumatano atarejea nchini kwa ajili ya kuendelea na mipango yake mingine, ingawa atarudi Marekani alikokuwa awali kuendelea na mazoezi.

"Nitarudi nyumbani siku mbili hizi, kuna vitu nakuja kuvifanya huko, lakini pia nitakuwa najifua hapo kisha kambi yangu itaahamia Marekani kidogo, nitafanya hivyo hadi Januari nitakaporudiana na Smith," amesema.