Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kijiwe kinaitakia kila la kheri Simba Zenji

KIJIWENI Pict

Muktasari:

  • Katika hili, bosi ni CAF ambayo ndiye tayari imeshaamua kuwa Simba na RS Berkane mechi yao ikapigwe Zanzibar badala ya Dar es Salaam iwe ni kwa sababu sahihi au hata za figisu hakuna namna ndio imeshaamua na hakuna namna ngoma inaenda kupigwa Zenji.

MNYAMA kapambana sana ili mechi yake ya marudiano ichezwe kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa badala ya New Amaan Complex, lakini ndivyo hivyo tena, bosi siku zote hakosei na huwa yuko sahihi.

Katika hili, bosi ni CAF ambayo ndiye tayari imeshaamua kuwa Simba na RS Berkane mechi yao ikapigwe Zanzibar badala ya Dar es Salaam iwe ni kwa sababu sahihi au hata za figisu hakuna namna ndio imeshaamua na hakuna namna ngoma inaenda kupigwa Zenji.

Jambo la msingi ambalo linaendelea hapa kijiweni kwa sasa ni kuiombea Simba na kutia ubani ili iweze kupindua meza Zanzibar na kutwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu baada ya kupoteza mechi ya kwanza ugenini kwa mabao 2-0.

Katika soka huwa tunaamini hakuna ambacho kinashindikana, hivyo bila shaka mnyama atapambana kiume na kupata ushindi ambao utamuwezesha kubakiza ubingwa nyumbani na kumfanya awe timu ya kwanza ya Tanzania kuandika historia hiyo.

Kijiwe kinaamini kwamba Zanzibar ni sehemu ya baraka kwa Simba na uamuzi wa kupeleka mechi Uwanja wa Amaan ni kama unaisaidia timu hiyo inayopeperusha bendera ya Tanzania hivi sasa kwenye mashindano iliyopo na Wanasimba hawapaswi kuwa na wasiwasi wala presha yoyote.

Kitendo cha kucheza fainali katika Uwanja wa New Amaan Complex tunaamini kitaifanya Simba ifanye maandalizi kabambe ambayo yatakuwa chachu kwake kufanya vizuri tofauti na ingekuwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa ambao Simba ingebweteka na kutofanya maandalizi mazuri na makubwa ikiamini hapo inaweza kupata matokeo mazuri kirahisi.

Simba imeshawahi kukutana na milima migumu na mirefu zaidi ya huo wa RS Berkane na iliwahi kuipanda na kuandika historia hivyo hapa kijiweni tunajiandaa kwenda Zanzibar kuiunga mkono tukiamini haiwezi kutuangusha na itaheshimisha nchi.

Historia ya kupata ushindi mnono wa mabao 5-0 ugenini, huku ikiwa imefungwa mabao 4-0 katika mechi ya kwanza nyumbani inapaswa kuwa chachu kwa wachezaji wa Simba kuikabili RS Berkane kibabe.