Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mudrick mambo yamnyookea Uturuki

MUDRICK Pict

Muktasari:

  • Nyota huyo alicheza ligi ya Uturuki baada ya timu hiyo kumwona katika mashindano ya Kombe la Dunia yaliyofanyika nchini humo na kufanya vizuri.

BEKI wa Mersin inayoshiriki Ligi ya Walemavu Uturuki, Mudrick Mohamed amesema licha ya kuchelewa kujiunga na timu msimu huu, lakini waliipambania kutoka nafasi ya tisa hadi nne bora.

Nyota huyo alicheza ligi ya Uturuki baada ya timu hiyo kumwona katika mashindano ya Kombe la Dunia yaliyofanyika nchini humo na kufanya vizuri.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mohamed alisema alifika wakati timu hiyo tayari imecheza mechi tano na ilikuwa kwenye nafasi mbaya na walipambana hadi ikamaliza pazuri.

"Tunashukuru Mungu tumemaliza salama, tena nafasi nne za juu, nilichelewa kujiunga na timu, nimekuta tayari imecheza mechi tano, tulishinda moja tu na nne tumepoteza," alisema Mohamed

Aliongeza msimu huu amebadilishwa nafasi kutoka beki hadi kiungo na bado alionyesha kiwango kizuri ambacho kimekuwa na msaada kwa timu.

"Msimu wa kwanza nilicheza kama beki, lakini nashukuru nilipambana na msimu huu nilisogezwa chini, ni kazi yangu, mchezaji anapaswa kubadilika na hilo limenisaidia."

Kiraka huyo alijiunga na Mersin mwaka 2022 akitokea Sauri Parasport Club ya Tanzania na anakuwa mchezaji wa tatu kutoka Tanzania kucheza ligi hiyo baada ya Ramadhan Chomelo anayekipiga Konya Amputee na Shedrack Hebron wa Sisli Yeditepe.

Msimu wa kwanza alicheza mechi 16 akifunga bao moja na asisti tano na msimu huu akicheza kiungo alicheza mechi 12, akifunga mabao sita na asisti tisa.