Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtihani alionao Momanyi Pamba Jiji

Muktasari:

  • Momanyi ambaye anaongoza kwa mabao katika kikosi cha Pamba Jiji akifunga matano kwenye ligi msimu huu, kesho Alhamisi anatarajiwa kuiongoza safu ya ushambuliaji ya timu hiyo kuikabili Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa katika Uwanja wa KMC Complex, Dar.

MSHAMBULIAJI wa Pamba Jiji, Mathew Tegisi Momanyi amesema ana kazi kubwa ya kufanya kuikabili safu ya ulinzi ya Simba, lakini jambo kubwa kwake ni kuhakikisha anatumia makosa ya wapinzani wao kutikisa nyavu.

Momanyi ambaye anaongoza kwa mabao katika kikosi cha Pamba Jiji akifunga matano kwenye ligi msimu huu, kesho Alhamisi anatarajiwa kuiongoza safu ya ushambuliaji ya timu hiyo kuikabili Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa katika Uwanja wa KMC Complex, Dar.

Mshambuliaji huyo aliyetua Pamba Jiji katika dirisha dogo la usajili msimu huu akitokea Shabana FC inayoshiriki Ligi Kuu Kenya, ameliambia Mwanaspoti kuwa anafahamu Simba ni timu kubwa, hivyo anajipanga kimwili na kiakili kukutana nayo.

“Simba ina safu nzuri ya ulinzi lakini hilo halituumizi kichwa kwa sababu tayari tumejipanga kuhakikisha wanafanya makosa ambayo tutayatumia kuwaadhibu.

“Wote tunafahamu kuwa mpira ni mchezo wa makosa. Kwa hiyo tutakuwa makini sana na mabeki wa Simba ili tutumie nafasi zote watakazoziachia,” alisema na kuongeza:

“Hii ni mechi ya heshima kwani msimu uko mwishoni, hivyo ni lazima tupambane kwa nguvu zote kusaka matokeo mazuri.”

Pamba Jiji inayoshika nafasi ya 13 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 27, inakumbuka Novemba 22, 2024 ikiwa nyumbani Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza ilipoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Simba, hivyo Alhamisi ni nafasi ya kulipiza kisasi.

Hata hivyo, Pamba Jiji inakutana na Simba yenye mwendelezo mzuri wa ushindi hasa inapokuwa nyumbani kwani katika mechi 12 za nyumbani msimu huu kwenye Ligi Kuu Bara imepoteza moja pekee, ikishinda tisa na sare mbili.

Safu ya ulinzi ya Simba ndiyo imeonekana kuwa ngumu zaidi ikiruhusu mabao machache zaidi ambayo ni tisa.