Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtibwa yatetea ubingwa U-20

Dakika 120 zimeweza kuamua ubingwa wa fainali ya ligi ya vijana chini ya miaka 20 na Mtibwa Sugar kufanikiwa kutetea ubingwa mara ya tano hii leo  dhidi ya Geita Gold katika uwanja wa Azam Complex Chamazi

Fainal hiyo ulimalizika kwa ushindi wa bao 1-0, Athuman Makambo akaifungia Mtibwa bao lake la Saba na kuibuka kinara wa mabao Ligi ya  Vijana chini ya miaka 20.

Mtibwa Sugar yakomba kila kitu Ligi Kuu ya Vijana U-20, kuanzia Kombe la ubingwa, mfungaji bora, kipa bora na mchezaji bora.

Mfungaji Bora, Athuman Masumbuko 'Makambo' kafunga mabao saba, likiwemo lililowapa Mtibwa Sugar ubingwa tano mfululizo kwa kuilaza Geita Gold usiku huu ndani ya dakika za nyongeza

Kipa Bora Toba Kutisha na Mchezaji Bora ni Ladaki Chasambi aliyetetea kwani msimu uliopita aliibeba.

Michuano hii ilianza 2008 na Mtibwa imebeba mara tano katika fainali tano mfululizo ilizoingia.